Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, katikati mwenye kofia akipata chakula na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sofia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu, Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Tale Tale pamoja na wananchi wengine katika mgahawa wa mama lishe katika Kibanda cha Rehema Shomali kata ya Kinole Mororgoro Vijijini akiendelea na ziara yake mkoani humo. Leo tarehe 3 Februari, 2023. (Picha na Fahadi Siraji CCM).
KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameyataka mabaraza ya madiwani nchini kufanya kazi za kujadili maslai ya wananchi na sio kurumbana kwa maslai yao binafsi.
Katibu
mkuu Chongolo alisema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa
CCM katika kijiji cha Kinole, jimbo la Morogoro kusini Mashariki ikiwa
ni muendelezo wa ziara yake ya siku tisa Mkoani Morogoro yenye lengo la
kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo.
"Madiwani kazi yenu ni kujadili hoja zenye tija na sio kuvutana bila sababu za msingi" alisema.
Alisema
amepata taarifa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Hamis Tale kuwa
Serikali ilipeleka fedha za kituo cha afya cha Kinole lakini fedha hizo
ziliondolewa baada ya kutokea marumbano wapi kituo hicho kijengwe.
"Naenda kuziwekea msisitizo fedha hizo zirudishwe ndani ya miezi miwili fedha zitakuwa zimefika "alisema..
Akizungumzia
elimu Chongolo aliwataka wazazi katika wilaya ya Morogoro vijijini
kuacha tabia za kuwafundisha watoto mambo ya wakubwa kabla ya umri wao.
"Zamani mtoto wa kike akimaliza darasa la saba anachezwa ngoma kisha anaolewa, acheni kuwafanya watoto wa kike mahari"alisema
Pia
aliwataka wazazi hao kuacha kuwageuza watoto kike kuwa wafanyakazi
wa ndani na badala yake wawapeleke shule ili waweze kuhudunia familia
zao kwa tija.
Kwa upande wa Afya, katibu huyo aliwataka kuacha kujitibu kwa waganga wa jadi na badala yake watumie huduma za vituo vya afya.
"Serikali
imewekeza fedha nyingi katika vituo vya afya na hospitali hakuna sababu
ya kwenda kutibiwa kwa waganga wa jadi"alisema.
Awali
katibu wa shina namba 2 Shomari Mkude alisema katika vikao vyao vya
shina hujadili kuhusu masuala ya kilimo na kumuhakikishia Chongolo
wanatarajia kuvuna mazao ya kutosha ifikapo mwezi Aprili na hivyo
hawatakuwa na njaa.
Pia
katibu huyo wa tawi alisema wanamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan
kwa kuwaletea madarasa mapya ya kutosha hali itakayowafanya wanafunzi
kusoma vizuri .
Katibu huyo wa tawi alitaka kujua kuhusu ujenzi wa barabara ya kutoka Bigwa hadi Kisaki kwa kiwango cha lami unaanza lini.
Akijibu
hoja hiyo meneja wa wakala. wa barabara mkoa wa Morogoro Alinanuswe
Kyamba alisema Machi 8 watafungua zabuni ya barabara hiyo ambapo kufikia
mwezi mwaka huu mkandarasi atakuwa ameanza kazi.
Kwa
Upande wake Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni, Issa
Haji Gavu amewasisitiza Wana CCM na wananchi kwa ujumla kuendelea
kuzalisha chakula cha kutosha ili kuwa na uhakika wa chakula.
No comments:
Post a Comment