*Yataka ushirikiano, uwajibikaji ngazi zote
*Timu ya Cross Country kuagwa Februari 14
Rais wa RT, Silas Isangi (katikati), akiteta na wadau katika moja ya matukio ya mchezo wa riadha.
NA TULLO CHAMBO, RT
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limeanika matukio manne makubwa ya kimataifa yanayolikabili mwaka 2023 na kusisitiza uwajibikaji wa pamoja kwa ngazi zote ili kuleta matokeo chanya.
Akizungumza na Wanahabari jijini Mwanza Februari 3, Rais wa RT, Silas Lucas Isangi, ameyataja matukio hayo ni Mashindano ya Mbio za Nyika 'Cross Country' ya Dunia, Bathurst, Australia Februari 18, Mashindano ya Vijana Afrika Mashariki (EAAR), U 18 na 20 Tanzania itakuwa mwenyeji Machi 10-11.
Tukio la tatu, Isangi alitaja ni Mashindano ya Afrika U 18 na 20 Lusaka Zambia Aprili 27 hadi Mei 3.
"Pia kuna mashindano ya Common Wealth U 18 huko Trinidad na Tobago Agosti 4-11, vile vile All Africa Games Julai 4-23 nchini Ghana na Mashindano ya Dunia Budapest, Hungary" alisema na kuongeza.
Kwa kifupi mwaka huu uko bize sana, hivyo viongozi wa Riadha ngazi za chini kabisa, lazima wote tuamke na kutimiza wajibu kwa vitendo.
Rais Isangi, aliitaka mikoa yote ifanye mashindano ya vijana ili kufanikisha upatikanaji wa timu ya Taifa U 18 na 20 yenye tija. Pia ushiriki wao kwenye mashindano ya Taifa uwe wenye tija.
TIMU YA TAIFA CROSS COUNTRY
Rais Isangi, amesema timu hiyo imeanza kambi toka Februari Mosi katika Hoteli ya Mvono, Ngaramtoni jijini Arusha kwa gharama za shirikisho asilimia 100.
Amesema, timu itakaa kambini hadi Februari 12,
[2:45 PM, 2/3/2023] Tullo Vd: itakapokwenda jijini Dar es Salaam tayari kwa kuagwa Februari 14, kabla ya kukwea pipa kwa safari ya Australia.
Amesema timu hiyo itakuwa chini ya Kiongozi wa msafara, Wakili Jackson Ndaweka ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu RT, Kocha Denis Male, huku wachezaji ni Mathayo Sombi, Inyasi Sulle, Fabian Nelson na Josephat Gisemo.
"Maandalizi yote yamekamilika ikiwamo tiketi, visa na vibali vyote vya serikali vimekamilika," alisema na kuishukuru serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kwa kusaidia katika maandalizi hayo.
No comments:
Post a Comment