Na Lydia Lugakila, Kagera
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe, Erasto Sima amewaagiza Maafisa Usafirishaji Maarufu (Boda Boda ) Mkoani Kagera kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vya uhalifu au kushiriki katika viendo hivyo kutokana na kubeba watu wasio waaminifu katika vyombo vyao.
DC Erasto ametoa kauli hiyo akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika mkutano uliowajumuisha zaidi ya Boda Boda 400 ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukoba uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba uliolenga kujua hali ya Chama Cha ushirika wa Boda Boda hao Masuala ya Mikopo, Pamoja na Masuala ya usalama Barabara.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kumekuwepo na baadhi ya Boda boda wasio waaminifu ambao wanatumika katika uharifu kutokana na kushirikishwa na abiria wanaowabeba katika Vyombo vyao.
"Uwe unamjua Abiria uliybeba au Haumjui nakushauri mpeleke anakokwenda akikushirikisha kwenye uharifu usishirikiane naye kwani ikibainika ukakamatwa hadi kufikishwa Mahakamani, Wewe uliyeshirikiana na muhalifu kwenda kuiba utahukumiwa zaidi kuliko muhalifu huyo" alisema Kiongozi huyo.
Aidha amewataka kuzingatia Sheria wawapo Barabarani ili kuepuka ajali ambapo amedai kuwa hakuna atakayevumiliwa endapo atakiuka Sheria.
Katika hatua nyingine amewasisitiza kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na nidhamu ikiwa ni pamoja na kutumia vyema Pikipiki za mikopo kabla hawajazimiliki moja kwa moja.
Amewahimiza kujenga utamaduni wa kurejesha fedha za Mikopo ya Pikipiki kwa wakati ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwani watakaofanya hivyo watampa kazi ngumu ya kuanza kuwafuatilia.
Haya hivyo amesema kuwa tayari Rais Dkt Samia kamuamini na kumtuma akawahudumie wananchi wa Wilaya hiyo hivyo atamsaidia kwa nguvu zote kutokana na kuwa hakuja Kagera kuwa Mkuu wa Miti pekee.
No comments:
Post a Comment