Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima akimfariji mume wa marehemu.
Marehemu Khadija Ismail enzi za uhai wake.
Na Lydia Lugakila
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Erasto Sima amelaani vikali mauaji ya mke wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Nation Housing Kata ya Rwamishenye yaliyofanywa na Kijana mwenye Umri wa Miaka 22 aliyetambulika kwa jina la Pascal Kaagwa aliyemuua kikatili Bi. Khadija Ismail Mwenye umri wa Miaka 29 ambaye ni mke wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Nation Housing Kata ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba, Devidi Dominic kwa kumpiga na kitu kinachosadikika kuwa ni ubao butu baada ya kumbaka kisha kutokomea kusikojulikana.
Kwa Mujibu wa DC Erasto tukio hilo lilitokea Februari 13, 2023 majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni eneo la Mtaa wa Nation Housing Kata ya Rwamishenye.
Akizugumza na waandishi wa habari pamoja na waombolezaji baada ya kuifariji Familia ya marehemu Erasto ametaja kusikitishwa na tukio hilo ambapo ameiomba Familia hiyo kuwa tulivu ili kuona namna ya kuupumzisha mwili wa marehemu baada ya taratibu zote kukamilika.
Adha ametoa wito kwa Vijana pamoja na wananchi kwa ujumla kuacha vitendo vya kujichukulia Sheria mkononi.
Kwa upande wake mume wa marehemu Devid Dominic amesema kuwa mke wake amemuacha katika kipindi kigumu kwani ameacha watoto wawili.
"Nawaombeni Viongozi mnisaidie ili kumkamata aliyefanya Mauaji haya, nashangaa Mimi Kama Mwenyekiti wa mtaa nimekuwa mstari wa mbele katika masuala ya ulinzi katika mtaa huu na huwa nawafikia kwa wakati Wananchi wangu wanapokuwa na matatizo Sasa leo hii nimefanyiwa haya alitamka kwa Majonzi Makubwa" Mwenyekiti huyo.
Naye mjomba wa marehemu na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM kutoka kata ya Nyanga, Kaijage Josephati amesema kuwa amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa ambapo amewaomba wananchi pamoja na familia hiyo kuwa wavumilivu.
Naye wifi wa marehemu, Alice Dominic amesema kuwa "baada ya kuona ukimya alimuita wifi yake ndipo watoto wake wakawa wanalia kuwa njoo umuone mama kabakwa na Pasco nilipoenda nikakuta wifi yangu yupo kitandani amelala huku mwili wake ukiwa wazi umefungwa shingo na kuonekana ubao ambao umetumika kumpiga huku zikionekana damu" alisema wifi wa marehemu huyo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Bukoba amewataka Wananchi kuwa walinzi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuoa taarifa wanapo baini vitendo vya namna hiyo na kujiepusha kutoa taarifa zisizo sahihi zinazeta tahaluki kwa Wananchi.
Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani Kagera limetoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tukio hilo na kuwa wanaendelea kumtafuta kijana huyo ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
No comments:
Post a Comment