HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 07, 2023

JESHI LA POLISI LAZINDUA OPERESHENI UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO ILIYODHAMINIWA NA NMB

 


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Ramadhani Ng'anzi (katikati), akipeana mkono na Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya NMB, Martin Massawe (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukaguzi wa magari kuelekea Wiki ya Usalama Barabarani, ambapo benki ya NMB ni mmoja wa wadhamini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, ACP Michael Deleli na kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Meloe Buzema na wapili kulia ni Meneja Mwandamizi Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Sophia Benno. (Na Mpiga Picha Wetu).

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Ramadhani Ng'anzi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa operesheni ya ukaguzi wa vyombo vya moto.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Ramadhani Ng'anzi (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya NMB, Martin Massawe (katikati), wakati wa hafla ya uzinduzi wa operesheni ya ukaguzi wa vyombo vya moto kuelekea Wiki ya Usalama Barabarani. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Sophia Benno. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya NMB, Martin Massawe, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa operesheni ya ukaguzi wa vyombo vya moto ambapo Benki ya NMB ni moja wa wadhamini.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Ramadhani Ng’anzi, akionesha mfano wa stika wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukaguzi wa magari kuelekea Wiki ya Usalama Barabarani ambapo benki ya NMB ni mmoja wa wadhamini. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Na Mwandishi Wetu

 

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, kimejidhatiti kuhakikisha kinadhibiti ajali za barabarani, hususani zinazotokea nyakati za usiku na kusababisha vifo vya watu na majeruhi.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Ramadhani Ng'anzi, wakati akizindua Operesheni ya Ukaguzi wa Vyombo vya Moto - ikiwemo magari, pikipiki na bajaji nchi nzima ambapo watakagua leseni za madereva, stika na ubora wa chombo.

"Katika tathmini yetu tumegundua kuwa ajali nyingi zinazosababisha vifo hutokea wakati wa usiku asilimia kubwa magari ya kubeba mizigo kugongana na magari ya abiria na gari binafsi hivo operesheni yetu kabambe itafanyika muda wote," amesema SACP Ng'anzi.

Pia Ng'anzi amesema lengo la kufanya ukaguzi wa magari hayo ni kuona kwamba vyombo vyote vinavyotumika barabarani ni Salama wanapima umadhubuti wa gari kwa vigezo na mifumo yote ya magari kuanzia breki, mfumo wa umeme na ametoa maagizo kwa RTO wote nchi nzima watege maeneo Maalum ya ukaguzi wa magari na litaanza Februari 6, 2023 hadi Machi 13 siku ya kilele cha sherehe za Wiki ya Usalama Barabarani 2023.

"Wiki ya Usalama Barabarani inatanguliwa na ukaguzi wa magari na utoaji wa elimu kwa watumiaji wa barabara kwahiyo matarajio yangu madereva wote kuanzia yanayobeba abiria, mizigo, magari ya mafuta ,magari yanayobeba wanafunzi yaliyokaguliwa hivi karibuni,pikipiki,bajaji wanaweza kufika katika kituo cha Polisi kwaajili ya ukaguzi na Jeshi la Polisi litatoa hati maalumu kuonyesha kwamba chombo hiko kimekaguliwa na inavigezo vya kuingia barabarani "amesema SACP Ng'anzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Bima kutoka Benki ya NMB Martini Masawe  amesema Benki hiyo imetoa udhamini katika Operesheni Kabambe kwa kuwa wanaguswa na ajali zinazotokea hivyo wataendelea  kuunga mkono suala hilo ili kusaidia ajali zinapungua kabisa.

No comments:

Post a Comment

Pages