HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 07, 2023

RT YAPONGEZA UONGOZI MPYA TASWA


NA TULLO CHAMBO, RT


SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limeupongeza uongozi mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), na kuwatakia kila LA heri katika majukumu yao mapya.

TASWA ilifanya uchaguzi wake mkuu Jumapili, Februari 5 jijini Dar es Salaam, na kushuhudiwa Amir Mhando akichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya huku Wakili msomi, Alfred Lucas akiwa Katibu Mkuu.

Imani Makongoro alichaguliwa Katibu Msaidizi, Dina Ismail Mweka Hazina huku Wajumbe wa Kamati ni Timzo Kalugira na Nasongelya Kilyinga.

Kwa mujibu wa Msemaji wa RT, Lwiza John, wanawapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa TASWA kwa imani kubwa waliyoonyesha kwa viongozi hao na familia ya Riadha inawatakia kila la heri katika majukumu yao ya kila siku.

Lwiza, alisema RT inatambua mchango mkubwa wa sekta ya habari katika maendeleo ya mchezo huo, hivyo wanawahakikishia ushirikiano wa kutosha.

"Tumepokea kwa faraja matokeo ya uchaguzi wa TASWA, na tunawapongeza viongozi wapya huku tukitarajia ushirikiano wa kutosha katika kuhamasisha maendeleo ya Riadha Tanzania, kitaifa na kimataifa," alisema Lwiza na kuongeza.

RT milango ipo wazi kwa TASWA na wanachama wake, hivyo wasisite kuwasiliana katika masuala mbalimbali yahusuyo mchezo wa riadha.

No comments:

Post a Comment

Pages