Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas, akizungumza na wananchi kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 117 ya Kumbukizi ya Vita vya Majimaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria Dkt Joseph Mhagama wa kwanza kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakipata elimu kutoka kwa Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo Khadija Kawawa.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza na Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzania Rosatom Khadija Kawawa alipotembelea banda la kampuni hiyo.
NA STEPHANO MANGO, SONGEA
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameipongeza Kampuni ya Mantra Tanzania Rosatom inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium kwa juhudi zao wanazozifanya kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma
Akizungumza jana Mkuu huyo wa Mkoa alipotembelea banda la Maonyesho la Kampuni ya Mantra Tanzania kabla ya uzinduzi wa wiki ya kumbukizi ya miaka 117 ya Mashujaa wa vita ya Majimaji kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Mahenge mjini Songea alisema kuwa Kampuni ya Mantra Tanzania inapaswa kupongezwa kwa namna inavyoshirikiana na jamii kutatua changamoto zinazowakabili
Kanal Thomas alisema kuwa Kampuni hiyo wakiwa wadau muhimu wa maendeleo wameshiriki maonyesho ya wiki ya kumbukizi ya miaka 117 ya Mashujaa wa vita ya Majimaji kwa kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira migodini na shughuli za kijamii ambazo wamekuwa wakizifanya
Alisema kuwa licha ya kampuni hiyo kutoa misaada hiyo kwa kutambua nguvu za Wananchi lakini bado kampuni hiyo inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea maendeleo Wananchi wake ambapo hadi sasa miradi mbalimbali imefanyika na inaendelea kufanyika.
Akizungumza kuhusu ushiriki wa kampuni hiyo katika kumbukizi hizo Meneja uhusiano wa Mantra Khadija Kawawa amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishiriki maadhimisho hayo kila mwaka ambapo wanatumia fursa hiyo kueleza kwa kina shughuli ambazo zinafanywa mgodini na katika jamii
Kawawa alisema kuwa imekuwa ikijikita kwenye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii ambayo inaizunguka kwa kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira, elimu ya ujasiliamali na misaada mbalimbali katika sekta za afya, ujenzi wa miundombinu ya elimu, maji, na ofisi za Serikali na kufadhiri miradi mbalimbali kwenye jamii ambazo zinauzunguka mgodi
Alisema kuwa Kampuni hiyo kila mwaka imekuwa ikidhamini ligi ya Wilaya ambayo imekuwa ikishirikisha timu kutoka kata zote za Wilaya ya Namtumbo kwa kuwapa awadi washindi, pamoja na vifaa muhimu ya michezo wakati wa ligi
Alisema kuwa mashindano hayo yalianzishwa kwa lengo la kuwanufaisha wananchi na wakazi wa Namtumbo kwa mambo mbalimbali kama vile elimu,afya,maji,watu wenye mahitaji maalumu,michezo na utamaduni,madaraja na barabara na elimu ya usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment