Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Mbinga Mji wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa fedha na mabati na MBUNGE wa Jimbo la Mbinga Mjini Jonas Mbunda, wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Mbunge Betram Kapinga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbinga Mji Kelvin Mapunda, wa kwanza kulia ni Katibu wa Mbunge Jonas Mbunda Dotto Ponera wakiwa na viongozi mbalimbali
NA STEPHANO MANGO, MBINGA
MBUNGE wa Jimbo la Mbinga Mjini Jonas Mbunda amefanya hafla fupi ya kukabidhi fedha taslimu na vifaa vilivyonunuliwa kwa fedha za mfuko wa Jimbo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambazo ni bati 968 zenye thamani ya Tsh 31,944,000 Milioni na fedha taslimu Tsh milioni 21,200,000/= kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi mbalimbali
Akikabidhi vifaa na fedha hizo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mbinga Kelvin Mapunda kwaniaba ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Jonas Mbunda ambaye yupo kwenye shughuli za vikao vya bunge mjini Dodoma.
Mapunda alieleza furaha yake kama Kiongozi wa Halmashauri kuona changamoto zinazowasilishwa na Waheshimiwa Madiwani pamoja na wananchi zikipatiwa ufumbuzi wa haraka na viongozi amboa wanawategemea kuwasemea katika ngazi za juu.
Mapunda alisema kuwa mchanganuo wa Bati 968 kuwa kwenye Kata ya Luwaita -Zahanati ya Kijiji cha Tukuzi Bati 250, Kata ya Mbangamao -Ukimo shule ya Msingi Bati 140 , Zahanati ya Mikorola Bati 26 Kata ya Luhuwiko- Ofisi ya Mtaa Luhuwiko Bati 120, Kata ya Matarawe - Ofisi ya Mtaa Puguru 150, Kipika shule ya msingi Bati 30
Alifafanua kuwa Kata ya Bethrehem - Ofisi ya Kata Bati 120, Kata ya Mpepai - Luhangai S/M Bati 140 na kwamba jumla ya Bati hizo 968 Bei ya bati moja ni Tsh 33,000/= kwa gharama ya Bati 968= Tsh 31,944,000/=
Alieleza zaidi kuwa mchanganuo wa Fedha Taslimu,Kata ya Mateka - Ukarabati Tanga shule ya msingi 5,000,000, Kata ya Myangayanga - Kitunda S/M Renta 2,000,000/=, Kata ya Kilimani - Ukamilishaji Zahanati ya Nzopai Tsh 4,000,000/=Kata ya Kihungu- Zahanati Mloweka Renta 2,000,000/=
Alisema kuwa Kata ya Kitanda- Ofisi ya Kijiji Renta 1,5000,000/=Kata ya Kikolo - Nyumba ya mganga Renta 3,500,000/= Kata ya Mpepai- Mpepai S/M Renta 2,000,000/= Kata ya Luhuwiko- Ukarabati wa Ofisi 1,200,000/=.ambapo jumla ya fedha Taslimu Tsh 21,200,000/=.
Aidha alimpongeza Mbunge kwa kujitoa kwake kutembelea Kata na Vijiji/mitaa kwenda kusikiliza changamoto zao na kutafuta namna bora ya kutatua.
Alisisitiza Viongozi wa Kata na Vijiji /mitaa kusimamia vizuri fedha na vifaa vilivyotolewa ili ndani ya siku 21wananchi waone matokeo ya fedha na vifaa hivyo.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mbinga Enock Ndunguru alimpongeza Mbunge kwa matumizi sahihi ya fedha ya mfuko wa Jimbo jambo ambalo linachochea maendeleo ya wananchi kama ambavyo mfuko huo umekusudiwa.
Ndunguru pia aliwataka wananchi kumshukuru na kuendelea kumpa ushirikiano mkubwa Mbunge kwani anaonyesha bidii kubwa ya kutatua changamoto zao.
Naye Katibu wa Mbunge Simoni Ponera akiongea kwaniaba ya Mbunge alimpongeza Rais kwa kuongeza fedha ya mfuko wa Jimbo la Mbinga Mjini kutoka Milioni 34 hadi Milioni 58 kwani ongezeko hilo linampa Mbunge wigo mpana wa kutekeleza miradi mingi zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzo.
Aidha, Alimshukuru Rais kwa kutoa fedha zinazotekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Vituo vya Afya, elimu , maji ,Umeme n.k. pia alishukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao Mbunge anaoupata kutoka kwa Viongozi wa Chama na Serikali ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji/Mitaa jambo linalorahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Joseph Mdaka alisema kuwa Mbunge ameonyesha uwazi katika matumizi ya mfuko wa jimbo na kwamba ni funzo kwa wabunge wengine wawe wa wazi katika fedha na matumizi yake yawe ya kuchochea shughuli za maendeleo ya wananchi na kugusa mahitaji sahihi ya walio wengi
No comments:
Post a Comment