HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 28, 2023

MNYAMA SI MBWA ACHUKUA TATU UGANDA

Na Mwandishi Wetu


HATIMAYE Mnyama Simba aunguruma pale Uganda katika Dimba la St Mary's nyumbani kwa Vipers na kuondoka na alama tatu muhimu za kwanza katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kundi C.


Simba waliingia kwenye mchezo huo wakihitaji ushindi pekee Ili kufufua matumaini ya kufanya vizuri msimu huu licha ya kupoteza michezo miwili ya kwanza dhidi ya Horoya AC ugenini kisha wakapoteza nyumbani Benjamin dhidi ya Raja Casablanca.


Kwa jinsi timu zote mbili zilivyocheza, basi alama tatu ndio ilikuwa muhimu sana kuliko kitu kingine chochote , hakukuwa na mamlaka  ya mchezo , pasi zilipotea kirahisi sana kuna nyakati nyingi timu zote mbili ziliamua kwamba uwanja upo hewani kwa kupiga mipira ya juu zaidi 


Kwa aina ile ya mchezo basi msingi mkubwa ulikuwa ni mipira iliyokufa kupata goli na ndio Simba walitumia hapo hapo kitu ambacho kocha wa Vipers lazima atakuwa amechukia kwa aina ya goli lile lakini kwa Robertinho atapongeza matamanio ya wachezaji wake wawili kuushinda ule mpambano wa hewani.


Mpira wa kwanza kashinda mchezaji wa Simba ( Inonga ) mpira wa pili Phiri na mpira wa tatu Inonga kafunga hapo bila mchezaji yoyote wa Vipers kugusa Simba anapata bao la kwanza msimu huu ugenini baada ya dakika 270.


Vipers wakiwa na 4-4-2 , wakishambulia katika vipindi vyote viwili walikuwa wanaenda na idadi ndogo sana ya wachezaji ambapo ulitarajia wakiwa na mpira watakuwa 4-2-4 , hawakuwauliza Simba maswali yoyote magumu zaidi ya mipira ya juu tu 


Baada ya goli moja , Robertinho aliona ni ngumu kufunga la pili muhimu ni kuimarisha kiungo na ndio maana akaingia Erasto Nyoni kuwatoa Simba kwenye 4-2-3-1 na kwenda 4-3-3 ( Nyoni Kanoute na Mzamiru kwenye kiungo ) na Chama Saido na Kibu mbele.


NOTE 


Mechi haikuwa na mambo mengi sana ya kimbinu baina ya timu zote mbili, mchezo ulikuwa wa kawaida sana ila katika hatua kama hizi kama huwezi kucheza vizuri na kupata matokeo basi hakikisha umepata matokeo kitu ambacho Simba wamekifanya.


Kwa ushidi Simba anasogea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi C nyuma ya vinara Raja Casablanca wenye pointi 9 wakishinda mbili bila dhidi ya Horoya AC ambao wako nafasi ya pili na pointi zao nne na Vipers wakibuluza mkia na pointi moja kibindoni

No comments:

Post a Comment

Pages