HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 15, 2023

TBA yapokea Bilioni 54.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba watumishi

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) katika kipindi cha miezi 18, umepokea jumla ya Sh. bilioni 54.2 kutoka serikalini kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma.



Mtendaji mkuu wa TBA, Daudi Kondoro amebainisha hayo jana jijini hapo, alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za wakala huo kwa waandishi wa habari.

Amesema miradi hiyo ni pamoja na ule wa ujenzi wa nyumba 3,500 za watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni Dodoma ambao uliwekwa jiwe la msingi na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango Novemba 30, mwaka jana.


“Serikali imeshatoa jumla ya Sh. bilioni 15.5 kwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 150 ambao umefikia asilimia 81 na awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba 150 za awamu ya pili ukiwa umefikia asilimia tatu”alisema Kondoro
 

Amesema, mradi mwingine uliotekelezwa kupitia kiasi hicho cha fedha ni wa ujenzi wa nyumba 20, za viongozi jijini Dodoma ambao umegharimu Sh. bilioni tisa.


Aidha, amesema mradi huo ulitekelezwa ili kukabiliana na uhaba wa nyumba za makazi ya viongozi uliojitokeza mara baada ya serikali kuhamishia makao yake makuu jijini Dodoma ambao umeshakamilika kwa asilimia 100.


“Ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma katika eneo la Magomeni Kota, awamu ya kwanza na ya pili kwa gharama ya Sh. bilioni 7.8, ujenzi wa jengo la ghorofa nane lenye uwezo wa kuchukua familia 16 tayari limeshakamilika kwa asilimia 99 na awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la ghorofa 8 umefikia asilimia 25”alisema


Kondoro, amesema mradi mwingine ni wa ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Temeke Kota ambapo linajengwa jengo la ghorofa tisa linalochukua familia 144, na utekelezaji wake umefikia asilimia tisa na uragharimu kiasi cha Sh. bilioni 3.3.

 
Mradi mwingine ni umaliziaji wa ujenzi wa nyumba tano za majaji katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro, Mtwara, Kagera na Shinyanga, kwa gharama ya Sh. bilioni 2.4 na nyumba nne zimeshakamilika na kuanza kutumika.


“Ujenzi wa nyumba ya jaji Kagera unaendelea na umefika asilimia 30 ya utekelezaji na miradi mingine inayotekelezwa ni ukarabati wa nyumba 40, za viongozi jijini Dodoma, awamu ya kwanza na ya pili.


‘Ukarabati wa nyumba 30 jijini Dar es Salaam,ukarabati wa nyumba 66 za iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), pamoja na

ukarabati wa nyumba katika mikoa 20 zilizohamishiwa TBA kutoka TAMISEMI”amesema


Pia, amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 na 2022/23, TBA imetekeleza miradi mbalimbali kwa fedha za ndani ambapo jumla ya Sh. bilioni 8.6 zimetumika.


“Miradi iliyotekelezwa kwa fedha za ndani inajumuisha ujenzi wa jengo la ghorofa sita lenye uwezo wa kuchukua familia 12 katika eneo la Canadian Masaki ambalo limefikia asilimia 99 za utekelezaji kwa gharama ya Sh. bilioni 4.6.’alisema


Hata hivyo, amesema TBA, pia imeanza ujenzi wa jengo la ghorofa saba kwa ajili ya makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Ghana Kota jijini Mwanza ambalo lipo hatua ya uchimbaji wa msingi

No comments:

Post a Comment

Pages