HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 15, 2023

Jamiii yaaswa kuacha kukopa mikopo ya Kausha damu

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

 

JAMII meshauriwa kuacha kukopa mikopo ya umiza kiholela maarufu kama (Kaushadamu) na baadala yake wameshauriwa kuchukua fedha hizo kwa matumizi lengwa kwani wanawake wengi wamekuwa wakichukua mikopo na kufanya mambo ambayo hayaingizi kipato kama vile kulipa ada,ujenzi wa nyumba na fahari za mavazi.

 

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Being'i Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekekezaji wa majukumu na mafanikio ya baraza hilo .

 

Aidha amesema kutokana na hali hiyo Baraza limeona kunahaja ya wananchi kupatiwa elimu ya Fedha ili wasijikute wameingia katika mikopo hiyo umiza.

 

"Baraza lina majukumu ya kuwezesha kubuni, kupanga, kusimamia, kufuatilia, kutathmini na kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wa kiuchumi nchini na linafanya kazi kwa kufuata na kusimamia sera ya Taifa ya Uwezeshaji yenye nguzo mbalimbali"amesema Beng'i

 

 

Mkurugenzi huyo amésema hadi sasa kuna kampuni zaidi ya 1,770 za Kitanzania zilizopata tenda katika miradi ya kimkakati na kufafanua kuwa watanzania zaidi ya 83,000 wamepata ajira katika miradi ya.   kimkakati hapa nchini.

 

Amesema  baraza limekuwa likisimamia kampuni za ndani kupata tenda Katika miradi mikubwa na ya kimkakati inayoendelea hapa nchini ambapo jumla ya kampuni 1771 zimepatiwa tenda.

No comments:

Post a Comment

Pages