HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 28, 2023

WANANCHI WILAYANI KYERWA MKOANI KAGERA WAHIMIZWA KUTUMIA BIMA ZA AFYA KUOKOA FEDHA

Na Lydia Lugakila Kyerwa

Wananchi Wilayani Kyerwa wamehimizwa kutumia kujiunga  na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii au Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa ili kuokoa fedha nyingi ambazo wamekuwa wakitumia kutoka mfukoni mwao kabla ya kujiunga na mifuko hiyo.



Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Lewanga  Msafiri (pichani) wakati akizungumza  na mtandao huu Februari 28, 2023.


Lewanga amesema kuwa Wananchi ambao si wanachama wa mfuko wa Afya ya jamii au bima ya afya ya Taifa wamekuwa wakitumia fedha nyingi sana kutoka mifukoni mwao jambo ambalo huwapa changamoto ikiwemo kuchelewa kupata huduma sahihi na kwa wakati sahihi.


"Mwananchi ujikuta akitumia fedha nyingi pale anapoenda kupata huduma ya matibabu  ambapo mtu akienda lazima afike dirisha la kujiandikisha yaani Mapokezi atalipa na atalipia pia kadi, vipimo vya maabara, baada ya hapo umwona Daktari kisha atatakiwa kulipia dawa hivyo basi tambua kuwa kuna umuhimu wa kutumia bima ni Muhimu kwani huokoa fedha hizo" alisema Lewanga.


Amesema jambo la msingi ni kuhakikisha Wananchi wanakuwa wadau wa bima ya afya au kujiunga na Mfuko wa Afya ya jamiia (iCHF)mbapo kaya ya watu 6 itakaa pamoja na kuchangia kiasi cha Sh 30,000 kwa mwaka mmoja na kutibiwa katika ngazi ya vituo tofauti tofauti ndani ya mkoa na nje mkoa huku wakiwa hawalipii vipimo, dirisha, dawa na kuwa watahudumiwa kwa wakati.


Aidha ameipongeza Serikali kwa namna ambavyo inapambana na mchakato wa kuhakikisha bima ya afya inapatikana kwa Watanzania wote  na kuhimiza kila mtu kujiunga na Mifuko ya bima lengo ni kuhakikisha Wananchi wanapata  huduma ya matibabu sahihi katika vituo vyote vya kutolea huduma.


Ameongeza kuwa Wananchi wanatakiwa kuondoa dhana ya kuwaza juu ya upatikanaji wa dawa kwani Halmashauri hiyo ya Kyerwa ina vituo 39 vya kutolea huduma hivyo wasisubiri kuona ugonjwa unakuwa sugu wafike wapate huduma sahihi kwa wakati sahihi.


Hata hivyo amempongeza Rais Dkt Samia kwa namna anavyoendelea kuwajali wananchi Wilayani Kyerwa kwa upande wa Madawa na vitendea kazi.

No comments:

Post a Comment

Pages