HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 25, 2023

YANGA MGUU SAWA KUWAVAA REAL BAMAKO KESHO

Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC, Yanga SC wako Mguu sawa kuwavaa wenyeji wao hapo kesho, mchezo wa tatu wa hatua ya makundi kunako kundi D.



Yanga watashuka dimbani tena kesho huko nchini Mali wakiwa na mzuka wa kuwapasua Mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL TP Mazembe mchezo uliopigwa wikiendi iliyopita katika Dimba la Benjamin Mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao (3-1).


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mali, nyota wa Yanga wako katika hali nzuri na maandalizi ni bora kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Real Bamako.


Yanga wanashuka dimbani wakiwa na pointi tatu walizozivuna nyumbani wakiwa nafasi ya tatu ya kundi D nyuma ya vinara US Monastiry ya Tunisia nafasi ya kwanza na pointi zao nne, huku TP Mazembe wakiwa nafasi ya pili na pointi zao tatu na Real Bamako wakishika mkia na pointi moja kibindoni.


Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na wanahitaji matokeo chanya kwenye mchezo huo.


"Maandalizi yanakwenda vizuri kama ambavyo programu ya mwalimu inaelekeza na kila kitu kiko sawa hapa. Hali ya hewa ni nzuri kwa maana  haina tofauti na ya Dar es Salaam.


"Kubwa zaidi ni kuwataka mashabiki wetu kuendelea kuisapoti timu na kutuonbea Dua  Ili kesho vijana waamke salama kwenda kuwapa Raha Wananchi" amesema Kamwe.


Timu hiyo imefikia kwenye hotel yenye hadhi ya nyota tano inayoitwa Granada Hotel-Lamite ambayo ipo katika Mji wa Bamako.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Modibo Keita,Mali

No comments:

Post a Comment

Pages