Na Mwandishi Wetu
Wakati yakiwa yamesalia masaa kadhaa kuelekea mchezo wa tatu wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kundi C ambapo Vipers ya Uganda inawakaribisha miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati Simba SC jioni ya leo kunako Dimba la St Mary's yapo mambo kadhaa kuelekea mchezo huo.
Wakati Simba wakiwa wamepoteza michezo yao miwili ya kwanza, Vipers nao hwajashinda mchezo wowote kwenye Dakika 90 tangu Robertinho aondoke kikosini mara ya mwisho kushinda ilikua Desemba 22, 2022.
Jambo la pili ikiwa Simba haijafunga bao katika michezo miwili ya hatua ya makundi, Vipers wao hawajafunga bao kwenye michezo mitano (5) mfululizo Suluhu (0-0) 4 na kupoteza moja (1) dhidi ya Busoga United December 20, 2022.
Tatu Katika historia ya Uwanja wa St.Mary's Leo ndio mara ya kwanza kutumika Usiku, Haikuwahi kutokea kwasababu haukuwahi kua na taa hapo awali, Leo ndio kama ufunguzi.
Nne Mshambuliaji wao Yunus Sentamu ndiye kinara wa kupachika mabao kwenye kikosi cha Vipers akiwa na mabao 6 kwenye Ligi Msimu huu.
Na jambo la mwisho Wanakosa wachezaji wao muhimu watatu (3) mlinzi Jjuko Murshid, Mshambuliaji Lumala Abdul na kiungo Olivier Osomba na Marvin Youngman.
Swali ni je Mnyama Simba ataamka pale St Mary's kwa Vipers ama mambo yataendelea kuwa magumu ama wote wataendelea kusaga meno kwa kukosa matokeo chanya katika dakika 90 nyingine.
No comments:
Post a Comment