Na Victor Masangu, Kibaha
Baadhi
ya wanachama na viongozi wa chama Cha mapinduzi (CCM) kata ya
Misugusugu wamempongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji kwa
kutumia fedha za mfuko wa jimbo katika kuchagiza na kuchochea naendelea
katika sekta mbali mbali.
Wanachama
hao waliyasema hayo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya chama cha
mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji ambapo wamesema juhudi ambazo
anazifanya zimeweza kusaidia kutatua baadhi ya kero na changamoto
zilizopo.
Diwani wa kata
ya Misugusugu Upendo Ngonyani wakati wa kusoma taarifa yake ya
utekelezaji amesema kumefanyika mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu
kuboresha madarasa ambayo yamesaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi
kazi ambayo imefanywa na Mbunge.
Kwa
Upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema
ataendelea kushirikiana na wananchi katika kuwaletea maendeleo.
Pia
aliongeza atahakikisha kwamba anaweka mikakati kabambe kwa ajili ya
kupeleka uchumi katika maeneo mbali mbali ili kuweza kuwapa fursa
wananchi waweze kupata huduma muhimu.
"Mimi
nawaomba wananchi wa kata ya misugusugu ni vizuri kuweka mipango ya
pamoja na kushirikiana na wananchi katika kuwaletea uchumi pamoja na
kusimamia miradi mingine ya maendeleo,"alisema Koka.
"Tunataka
tutengeneze mtandao wa Kuhakikisha kwamba watu wa Tarura au Tanrods ni
lazima kwenda kwa wahusika ili kuweza kujua jinsi ya kutekeleza miradi
yao ya maendeleo kwa kushirikiana kwa pamoja,"aliongeza Koka.
Kadhalika
Mbunge huyo aliongeza anaendelea na juhudi katika kuboresha huduma ya
maji safi na salama katika maeneo mbali mbali kwa wananchi wa kata ya
misugusugu na maeneo ya viwanda na biashara.
Pia
alisema ataendelea kutekeleza ilani ya chama Cha mapinduzi kwa vitendo
na kusimamia fursa za ajira kwa vijana na kwamba lengo ni kuwakomboa
wananchi kiuchumi na kupata ustawi kwa pamoja.
Katika
hatua nyingine ameahidi kukivalia njuga baadhi ya watu ambao
wanakabiliana na changamoto ya kunyanyaswa na wenye viwanda ambao
wanafanya dhuruma kwa wafanyakazi wao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wiaya ya Kibaha
mji Mwajuma Nyamka amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wanachama
kuwa na makundi kwa ajili ya kupanga safu ya viongozi kabla ya uchaguzi
kufika kwani ni kinyume kabisa na utaratibu.
Pia
Nyamka aliongeza kuwa viongozi wa mashina wanapaswa kubadilika na
kuweka mipango ya kuongeza idadi ya wanachama ili kuweza kukiimarisha
chama pamoja na Jumuiya zake.
Ziara
ya kamati ya siasa ya chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji
imefanya ziara katika kata ya misugusugu kwa lengo la kuzungumza na
wanachama pamoja na kutembelea viongozi wa ngazi mbali mbali.
No comments:
Post a Comment