HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 04, 2023

RT YATEKELEZA MAAGIZO YA BMT


Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha, akipokea ripoti ya mapato na matumizi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), ya mwaka 2021/22 kutoka kwa Makamu wa Rais wa RT, William Kallaghe (kulia).


NA TULLO CHAMBO, RT


SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), leo Machi 3, 2022, limetekeleza agizo la Baraza la Michezo la Taifa (BMT), baada ya kukabidhi ripoti ya mapato na matumizi.

Ripoti hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Rais wa RT, William Kallaghe, kwa Katibu Mtendaji wa BMT, Neema Msitha.

BMT ilifanya kikao na Kamati ya Utendaji ya RT,  Januari 21 kwenye moja ya kumbi za Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, na moja ya maelekezo ya Baraza, ilikuwa ni kuitaka RT kuwasilisha ripoti ya mapato na matumizi 2020/21 hadi 2021/22.

Baada ya kuipokea ripoti hiyo, Katibu Mtendaji BMT, Msitha, alisema watakaa na kuifanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

Pages