Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Taasisi
ya Wahandisi Tanzania (IET) kwa kushirikiana na Chama cha Wahandisi
Washauri Tanzania (ACRT) na Bodi ya Usajili ya Wahandisi Tanzania
(EAFEO) ikiungana na Taasisi zote za Uhansisi Duniani kupitia Shirikisho
la Taasisi za Kihandisi la Afrika Mashariki (EAFEO) na Shirikisho la
Taasisi za Kihandisi la Afrika (FAEO) inatarajia kuadhimisha Siku ya
Uhandisi Duniani kwa Maendeleo Endelevu.
Akizungumza
na Wanahabari Jijini Dar es salaam rais wa Taasisi hiyo Mhandisi Dkt.
Gemma Modu amesema Maadhimisho hayo yatafanyika Machi 4 Mwaka huu katika
Ukumbi Karimjee jijini humo yakiwa yamebeba ujumbe wa "Ubunifu wa
Uhandisi kwa unaostahili zaidi " hiyo ni Kwa kuzingatia kuwa Dunia ipo
zama za utandawazi ya Karne ya 21 na utashi kwenye Uchumi na Jamii
zinazoendeshwa kwa nguvu ya Teknolojia ambayo maendeleo yake ni makubwa
na ya kasi .
Amebainisha kuwa
maadhimisho hayo ni fursa ya kuhamasisha na kuhimiza vijana wa kike na
kiume ambao ndio taifa la kesho kuingia kwenye uhandisi ili kuhakikisha
utekelezaji wa endelevu wa malengo ya maendeleo endelevu kwa miaka
mingi ya mbele na vizazi vijavyo.
"Madhumuni
ya siku hii ni kutoa fursa ya kutambua na kuthamini mchango wa
Uhandisi na watekelezaji wa kazi za Kiuhandisi wakiwamo Wahandisi na
Mafundi wote katika kuleta Maendeleo endelevu ya Taifa letu kwa ujumla
na kuboresha uelewa wa Umma kuhusu jinsi uhandisi wa Teknolojia ilivyo
na umuhimu Kwa maisha yetu ya kila siku katika ulimwengu wetu wa
Sasa"amesema rais Gemma
Gemma
amewasisitiza Wahandisi Mapinduzi ya kidigitali yanaandamana na ubunifu
wa sayansi huku matumizi yake lazima yalete tija katika uzalishaji wa
bidhaa,utoaji huduma na uendeeshaji wa Mifumo na utekelezaji wa
mikakati mbalimbali ya kukuza Uchumi kwa Maendeleo Endelevu kwani
hayategemei tu ujuzi ..
Ameongeza
kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na Washiriki zaidi ya
200 kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi ambapo zitapata fursa
ya kuonyesha bunifu zao katika kutekeleza miradi ya kimkakati
inayoendelea nchini huku wanafunzi wa vyuo na Sekondari watashiriki na
kuonesha bunifu zao za masomo yao.
Amewakaribisha
watanzania wote kujitokeza kwa wingi kwenye maadhimisho hayo kwani siku
hiyo ni muhimu duniani katika sekta ya uhandisi ulimwenguni na umma
kujua nini wahandisi na mafundi wanafanya kwa maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment