HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2023

KINARA WA MABAO SWPL ATIMKIA UTURUKI

Na John Richard Marwa

Mabingwa wa Ligi Kuu Soka la Wanawake Tanzania Bara, Serengeti Lite Women's Premier League (SWPL) Simba Queens wamefikia makubaliano ya kumuuza nahodha wa timu hiyo Opa Clement kwenda Besiktas ya Uturuki.

Opa anaondoka Simba Queens akiwa ndiye kinara wa mabao msimu huu ambao raundi ya pili inaenda kuanza kesho huku Simba ndio vinara wa Ligi hiyo wakiwa na alama 22 katika michezo tisa wakifunga mabao 29 na kuruhusu mabao matano.



Kwa mujibu wa taarifa ya Klabu ya Simba iliyotolewa kwenye Simba App imeeleza kuwa tayari mshambuliaji huyo ameshaondoka nchini kuelekea Uturuki kwenda kuanza maisha mapya ya Soka katika timu yake ya Besiktas.

"Mpaka Opa anaondoka Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women's Premier League) mzunguko wa kwanza umemalizika na yeye ndiye kinara wa ufungaji akiwa amepachika wavuni mabao tisa.

"Uongozi wa klabu ya Simba unamtakia Kheri Opa katika majukumu yake mapya na pia una mkaribisha muda wowote atakapoamua kurejea tena nyumbani." Imeeleza taarifa hiyo


No comments:

Post a Comment

Pages