Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Chama
cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kimewahimiza wanawake
wajasiriamali na wafanyabiashara kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani ambayo yanaambatana na Maonyesho ya Bidhaa mbalimbali
na Utoaji Tuzo kuanzia Machi 9 hadi 11 mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TWCC,Mwajuma
Hamza amesema katika sherehe hizo zitakazofanyika katika viwanja vya
mlimani city na baadaye kutolewa kwa tuzo katika ukumbi huo Macchi
11,2023 zenye lengo la kutambua na kuheshimu wanawake waliofanikiwa na
wale wanaochipukia katika sekta za viwanda na biashara.
Amebainisha
kuwa malengo mengine ya kutolewa kwa tuzo hizo ni pamoja na kujenga
imani juu ya ujasiriamali na kuhamasisha wanawake wa vizazi vijavyo
kuwekeza na kujishughulisha katika shughuli za viwanda na
biashara,pamoja na kusheherekea mafanikio wanayoyapata wanawake katika
sekta za viwanda na biashara hapa nchini.
Mwajuma
Hamza amesisitiza kuwa tuzo hizo ambazo zinatolewa kwa mara ya tatu pia
zinalenga kuonesha mchango wa mwananmke mjasiriamali katika kukuza
uchumi wa nchi kwa kuchoche maendeleo ya jamii.
"wanawake
ni nguzo muhimu katika maendeleo ya jamii yoyote na kwamba wanawake
wana uwezo wa kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda na
biashara endapo wataaminiwa na kupewa nafasi hiyo"aliongeza
Ameishukuru
serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini ambapo
wanawake wengi wameweza kuanzisha biashara na viwanda vidogo ambavyo
vimewaongezea vipato,kuzalisha ajira pamoja na kuchangia katika kukuza
uchumi.
"Kipekee
kabisa ninamshukuru Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa
anayoifanya ya kufungua nchi na kuboresha mazingira ya uwekezaji
nchini,sisi wanawake tumejipanga kikamilifu katika kutumia fursa vizuri
kupitia wiki hii ya viwanda ya wanawake ndipo tunapata nafasi ya
kujitathmini na kuweka mikakati ya kuendeleza biashara zetu"alisisitiza
Bi Mwajuma Hamza
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Africa (TMA), Monica Hangi
ambao ndiyo wadhamini wakuu wa tuzo hizo chini ya miradi wa kujengea
wanawake uwezo wa kufanya biashara Tanzania amesema TMA imetenga kiasi
cha Sh Bilioni nne kwa ajili ya mradi huo wa kuwawezesha wanawake
kufanya biashara.
Ameongeza
kuwa TradeMark Africa imeamua kudhamini tuzo hizo za wanawake kupitia
TWCC kwa lengo kubwa la kuhakikisha biashara za wanawake zinakuwa na
kuleta tija kwa Taifa kwani tuzo hizo zimekuwa zikitoa chachu kwa
wanawake wengi kutamani kuingia kwenye biashara.
"Wapo
wanawake wengi wanaojifunza kupitia wale waliofanikiwa na hii ndiyo
maana halisi ya hizi tuzo kuwatangaza wale wote waliofanikiwa na
wanaofanya vizuri kibiashara ili wengine waweze kujifunza"Ameongeza
Mkurugenzi Mkazi wa TMA Monica Hongi
No comments:
Post a Comment