Na Lydia Lugakila
Ikiwa Machi 9 ya kila mwaka ni siku ya Figo Duniani jamii yatakiwa kubadili mtindo wa maisha ili kuepuka magonjwa ya Figo.
Akizungumzia siku hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Lewanga Msafiri amesema kufanya mazoezi kwa dakika 30 angalau mara 3 kwa wiki kutasaidia kupunguza uwezekano wa kupata Magonjwa kama Kisukari, Shinikizo la damu, ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa magonjwa ya Figo.
Amesema Wananchi wanatakiwa kuepuka visababishi vinavyomfanya mtu kupata ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi, kula vyakula vyenye mafuta, Sukari au Chumvi kwa wingi, kuvuta Sigara au matumizi ya aina nyingine yeyote ya tumbaku na uzito kupita kiasi.
Lewanga amezitaja kuwa Dalili za ugonjwa wa Figo kuwa ni shida katika kipata aja ndogo, kupungua kwa mkojo au kutopata mkojo kabisa, kukojoa damu, maumivu ya tumbo, kuvimba mwili na kukosa nguvu.
Aidha amewaomba Wananchi Wilayani Kyerwa pamoja na Watanzania kwa ujumla kubadili mtindo wa maisha na kufika vituo vya kutolea huduma wanabaini dalili za ugonjwa huo ili wapimwe mkojo, wingi wa damu, kemia ya damu, sukari,na kupata matibabu sahihi.
Hata hivyo siku ya Figo Duniani huadhimishwa Machi 9 ya kila mwaka ambapo kwa mwaka 2023 siku hiyo imechagizwa na kauli isemayo " Afya ya Figo - kujitayarisha kwa yale yasiyotarajiwa, kusaidia walio hatarini".
March 09, 2023
Home
Unlabelled
JAMII KAGERA YATAKIWA KUBADILI MTINDO WA MAISHA KUEPUKA UGONJWA WA FIGO
JAMII KAGERA YATAKIWA KUBADILI MTINDO WA MAISHA KUEPUKA UGONJWA WA FIGO
Share This

About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment