HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 04, 2023

Mchora katuni Said Michael ‘Wakudata’ alivyomchora Nabii Mkuu Dkt. GeorDavie


 Na Mwandishi Wetu

 

Mchora katuni maarufu nchini, Said Michael maarufu kwa jina la Wakudata, ambaye amekuwa akichora katuni zenye ujumbe mzito na za kuelimisha, kuibua mijadala ya maendeleo katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya nchi amechora katuni mbalimbali zinazoeleza matukio na kazi za Nabii huyo na kukitolea kitabu.


Kitabu hicho chenye  maoni na maudhui yanayoonesha kazi za Nabii Mkuu Dkt GeorDavie,  ambacho kimepewa jina la KIBOKO YA SHETANI, kilichosheheni katuni za Nabii huyo maarufu jijini Arusha na nchini kwa ujumla kinatarajiwa kuanza kuuzwa jumapili tarehe 05 Machi 2023 Ngurumo ya Upako Kisongo Arusha.

 

Kitabu kina katuni zenye misisimko, mafundisho  na kuonesha ukuu wa Mungu katika kazi za Mtumishi huyo wa Mungu, mwanzilishi wa huduma ya NGURUMO YA UPAKO, kilizinduliwa jijini Arusha hivi karibuni na kiongozi huyo wa kiroho ambaye pia amekuwa akisaidia watu mbalimbali kujikwamua kiuchumi.


Pia kijitabu hicho kimeandikiwa Dibaji na mwandishi wa siku nyingi, Deogratius Temba, ambaye ameeleza na kuweka mkazo juu ya umuhimu wa kijitabu hicho na maudhui yake, na amewataka wasomaji wahakikishe wanakisambaza kwa watu wengi zaidi, ili kuendeleza kazi nzuri ya Nabii Mkuu Dkt. GeorDavie.

 

Kijitabu hicho, chenye ujumbe mzuri unaovutia na kueleweka kwa urahisi, kitauzwa kanisani NGURUMO YA UPAKO Kisongo jijini Arusha na sehemu mbalimbali Tanzania kwa gharama ya Tsh. 3,500 tu.


Said Michael maarufu kwa jina la Wakudata

 


No comments:

Post a Comment

Pages