HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 01, 2023

VINARA WA KUFUMANIA NYAVU WA MACHAMP ION SOKA LA WANAWAKE

Na John Richard Marwa

Wakati Ligi Kuu Soka la Wanawake Tanzania Bara SWPL ikitarajiwa kuendelea mzunguko wa pili msimu huu wa 2022/2023. Simba Queens bado wako kwenye mbio za kutetea taji lao kwa msimu wa nne hawa ndio vinara wa kufamania nyavu kwa Mabingwa hao.

Simba wamemaliza mzunguko wa kwanza kwa kukusanya pointi 22, wakishinda mechi saba sare moja na kupoteza mmoja. Wamefunga mabao 29 huku wakiruhusu nyavu zao kutikisika mara tano.



Katika mabao hayo 29 yamechagizwa na nyota wanna ambao wamekuwa na wastani mzuri wa kufumania kamba za wapinzani. Opa Clement amefunga mabao tisa wastani wa bao moja kwa kila mechi.

Wa pili ni Jentrix Shikangwa amefunga mabao saba wastani wa 0.777.... Kwa kila mechi. Asha Djafar ameingia kambani mara nne wastani wa 0.444.... huku Vivian Corazone nae akifunga mabao manne wastani wa 0.444.... kwa mechi.

Wanna hao wameingia kambani mara 24 kati ya mabao 29 ambayo Simba Queens wameyafunga katika raundi ya kwanza ya msimu huu.

Swali ni je nyota hao wataendelea kuwa kwenye huo ubora kwa raundi ya pili kuisaidia Simba Queens kutetea ubingwa wao kwa msimu wa nne mtawalia? Simba Queens watashuka dimbani March 8 kumenyana na JKT Queens katika Dimba la Meja Generali Isamuyo Mbweni jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

Pages