Na Mwandishi Wetu
Baada ya kuwepo kwa taarifa juu kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Mohammed Nasreddine Nabi anawindwa kupewa kibarua cha kuwa kocha wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars' mwenyewe ameibuka na kutolea ufafanuzi.
Katika mahojiano ambayo Kocha Nabi ameyafanya na gazeti namba moja la michezo nchini la Mwanaspoti.
Nabi ameliambia Mwanaspoti kuwa anafurahia kupewa nafasi kubwa kama hiyo ya kuifundisha Taifa Stars lakini kwasasa ni vigumu kukubali ofa hiyo.
Nabi amesema kwasasa ajira pekee ambayo anaweza kuifanya akiwa ndani ya ardhi ya Tanzania ni kuendelea kuifundisha Yanga.
"Nimeona hizo taarifa lakini hata familia yangu wameshtuka walipoona lakini niwashukuru wanaonifikiria kuhusu nafasi hiyo,"amesema Nabi.
"Naomba waambie mashabiki wa Yanga kwamba mimi kwa hapa Tanzania kwasasa nitaifundisha timu yao pekee mpaka nitakapochukua uamuzi mwingine," amesema Nabi
"Sina maana kwamba kuifundisha Tanzania ni kazi mbaya kwangu hapana lakini huwa Nina utaratibu wa kumaliza jambo ambalo nimelianza," amongeza Nabi
No comments:
Post a Comment