HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 14, 2023

CHUO KIKUU MZUMBE YAENDESHA SEMINA YA AFYA KWA VIJANA


 Kaimu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Coretha Komba, akitoa hotuba yake wakati akifungua semina ya Afya kwa Vijana iliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Tegeta na kuwashirikisha zaidi ya wanafunzi 400.
Baadhi ya washiriki.

Muuguzi wa Kituo cha Afya Buguruni, Janeth Nyera, akitoa mada wakati wa semina wakati wa semina ya Afya kwa vijana iliyoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Slyvester  Salasini akichangia mada katika semina hiyo.

 

 

 Rais wa Wanafunzi Ombeni Kisuka, akizungumza wakati wa semina hiyo.

 

 Muuguzi wa Kituo cha Afya Buguruni, Janeth Nyera (kushoto) akiwa katika maandalizi ya kumpima HIV Mbunge wa Bunge la Wanafunzi, Shamim Said wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakati wa semina ya Afya kwa vijana iliyoandaliwa na chuo hicho.

Dk. Deodatha Lyochi kutoka Shirika la MDH akitoa mada wakati wa semina ya Uelimishaji na Uhamasishaji wa kujinga na ueneaji wa maambukizi ya VVU iliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Tegeta jijini Dar es Salaam.





Na Mwandishi Wetu

Chuo kikuu cha Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Tegeta kimeendesha semina ya afya kwa vijana kuweza kutambua hali zao za kiafya na namna ya kujikinga na magonjwa ya zinaa pamoja na Ukimwi.

Semina hiyo imefanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo imefunguliwa na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Coretha Komba amewataka vijana kuzingatia mafunzo hayo Ili kulinda afya zao kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

"Hii semina ni nzuri imebeba mafunzo muhimu sana katika maisha yetu, tukiharibu kwenye  haya tutakapofundishwa leo hata hiyo BPA hatutaiona nzuri sana, haitatufaa sana labda.

"Sasa hapa wapo kwa malengo mawili, la kwanza kutufundisha kuna wengine labda wanafahamu haya wanayokuja kutufundisha lakini kuna wengine hawayafahamu kabisa, kwa hiyo ni vizuri kukaa kusikiliza lakini watatufundisha jinsi ya kujikinga kama ambavyo bango letu limeandikwa jinsi ya kujikinga lakini tunaambiwa kwamba huu ukimwi hata ukiwa nao sio mwisho wa maisha kwa sababu baada ya hapo tutatakiwa kupima ambayo ni hiari." amesema na kuongeza kuwa.

"Lakini mimi nawashauri sana ni vizuri sana kupima kwa sababu ukijua utajua uishi vipi, kwaiyo mimi nawatakia mafunzo mema lakini nawahamasisha pia sana, Mimi pia nikitoka hapa naenda kupima kwaiyo nawahamasisha sana na nyie mpime kwa sababu ukipima ndio mwanzo wa kufanya vizuri katika maisha yako kwamba utajua uko katika hali gani Ili ujiepushe au ili uishi vizuri sasa kulingana na hali yako majibu yako.

"Kwaiyo kitu chochote ni kizuri kujua uko positive ama negative ni vizuri kusudi ujue baada ya hapo unajipanga vipi Ili uishi vipi baada ya kujua hali yako." amesema Dk. Komba.

Lakini kwa upande wa mtoa mada katika semina hiyo, Muuguzi na mshauri wa masuala ya unyanyaji wa kijinsia, Janeth Nyela amesema mafunzo hayo yatawasaidia sana vijana kwa sababu ni kundi ambalo linakumbana na changamoto za afya na unyanyasaji wa kijinsia.

"Tumekuja kwa ajili ya kuongea na vijana na kutoa mafunzo, nashukuru tumeongea na vijana wameweza kuelewa na kuwafundisha masuala ya vijana ni nini, umuhimu wa kupima, umuhimu wa kujua afya zao kwa sababu afya ni mtaji na pamoja na upimaji pia.

"Kwa hiyo naona uongozi mzima wameweza kulichukulia na kulipa kipaumbele kwa kujua kwamba vijana kama tunavyosema asilmia kubwa Tanzania nguvu kazi tunaangalia vijana kwa sababu hao ni nguvu kubwa hivyo wametuita Ili kutoa huduma hizo." amesema na kubainisha kuwa.

"Huduma zimeenda vizuri kama mlivyoona, vijana wamefika kwa wingi kwa ajili ya kusikiliza masomo pamoja na kupima na kusikiliza ushauri.

"Semnina hii itawasaidia sana kama nilivyosema kwamba vijana ndio nguzo ya Taifa kwa maana hiyo itawasaidia katika kuboresha afya zao kama tulivyosema asilimia kubwa wao ndio wanaongoza kwenye masuala ya magonjwa ya zinaa na ukimwi kwa pamoja kwaiyo somo hili litawasaidia sana kujua kijana jinsi gani aweze sasa kujitunza katika maisha yake hasa kwa upande wa afya.

"Vijana wengi wako Vyuo na huku hawana Elimu kubwa sana ya namna ya kujikinga, na kwa sasa hivi namba kubwa ya maambukizi iko kwa vijana ndio maana tumeamua kupita vyuoni kuweza kuwaelimisha namna gani ya kuweza kujikinga." amesema Janeth Nyera.

No comments:

Post a Comment

Pages