HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2023

DKT. JAKAYA KIKWETE AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUFTURISHA YATIMA NA WAJANE KIBAHA

Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akizungumza kwenye hafla ya  Iftar iliyofanyika Kibaha  nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani  jana usiku Aprili 12.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge  akizungumza kwenye Iftar hiyo  hafla iliyofanyika Aprili 12   nyumbani kwake Kibaha Mkoani Pwani.

 Baadhi ya Watoto yatima waliohudhuria Iftar hiyo.
Kutoka kushoto ni Afisa Habari Mkoa wa Pwani  Nasra Mondwe na mwandishi wa habari Khadija wakiwa kwenye foleni ya kupata Iftar.

 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akiwa na katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo ya iftar.

 

Na Khadija Kalili

RAIS Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  ametoa shukrani za dhati kwa  Mheshi miwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuandaa ftari kwa wajane na yatima walioko Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Dkt. Kikwete amesema hayo jana usiku Aprili 12 mwaka 2023 alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Iftar  iliyoandaliwa Ofisi  ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuongozwa  na RC Alhaji  Abubakari Kunenge.

"Nasema dhahiri kwamba  haikuwa chaguo kwa  Watoto hawa kukosa wazazi wao bali ni mipango ya Mungu na kina mama wajane kupoteza waume zao  lakini kwa ajili ya watu wema  na wacha Mungu walioamua kuwakumbuka kuwafturisha leo tumekutana hapa kupata ftari pamoja nao hii ni ishara ya upendo wa hali ya juu, niseme tu sisi wengine tumekuja kukuunga mkono RC Kunenge katokana na jambo hili kubwa la ibada la kukumbuka yatima umefanya kama jinsi ulivyosema kuwa Iftar hii imeandaliwa na Mheshimiwa Rais wetu Kipenzi chetu Dkt. Samia  Suluhu Hassan, tunamshkuru sana  kwa moyo wake  wa upendo, ukarimu na kuwakumbuka watoto yatima na wajane,amesema Dkt. Kikwete.

"Rais ana mambo mengi ya kufanya ikiwamo pamoja na kulitumikia taifa lakini ameweza kukumbuka kufanya ibada ya kufturusha kundi hili muhimu katika jamii nampongeza sana" amesema Dkt. Kikwete.

Amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kumuombea kwa Mwenyeezi Mungu amjaalie afya  njema Rais Samia umri mrefu ili aendelee kuliongoza Taifa la Tanzania kwa amani na utulivu huku akizitatua changamoto za wananchi kwa hekima ya hali ya juu.

Aisha Rais Mstaafu wa awamu ya nne  Dkt. Kikwete amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Kunenge kwa kuuongoza vema Mkoa wa Pwani kutokana na jinsi anavyojali maslahi mapana ya wananchi wa Mkoa huu,ikiwa ni pamoja na kujali maendeleo  ya wananchi  huku akimuombea dua Mwenyeezi Mungu amuwezeshe  kumpa uwezo wa kimwili na kiakili ili aweze kutimiza yote mema  aliyodhamiria  kuyatenda kwa wan Pwani na mwisho amemshkuru kwa mualiko wa Iftar hiyo.

RC Kunenge akizungumza kwenye Iftar hiyo amesema  kwa kuwaeleza wakaazi wote wa Pwani kutumia vema fursa zilizopo ndani ya Mkoa hasa Viwanda na Biashara  katika kujiletea maendeleo. "Kila mtu awe mchungaji wa mwenzake katika jamii na hili ni jukumu la wote kwani  hasa hivi sasa  Dunia imegubikwa na utanda wazi na  janga la maadili yanayokwenda kinyume na maadili ya dini pamoja na mila zetu hata katika vitabu vitakatifu vimepinga ikiwemo,Torati,Zaburi,Injili na Qur'ani tuwalinde watoto wetu ili kesho kwa Mwenyeezi Mungu tukapate maskani mema kwa sababu tukishindwa kukilinda kizazi chetu tutakwenda kuulizwa kwa Mola wetu" amesema RC Kunenge.


Iftar hiyo imehudhuriwa na viongozi kutoka Serikalini wakiwemo  Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani, Wakurugenzi  na Viongozi kutoka katika madhehebu mbalimbali ya dini,viongozi wa Vyama vya siasa ikiwemo  Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Kamati ya Ulinzi na UsalamaMkoa wa Pwani , Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani  pamoja  watu binafsi.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Pages