HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2023

MABINGWA WA CAF BUNGENI

Mabingwa wa Afrika  wa Mpira wa Miguu kwa Shule za Sekondari ambao ni Shule  ya Fountain Gate wakiwa Bungeni jijini Dodoma kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Aprili 13, 2023.



Mabingwa hao wameambatana na Viongozi mbalimbali wa Wizara na  Taasisi wakiongozwa na Katibu Mkuu Saidi Yakubu FCG, Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania wakiongozwa na Rais wa TFF, Wallace Karia pamoja na viongozi wa Fountain Gate.


Mabingwa hao ambao pia ni mabingwa wa CECAFA walitwaa  Kombe hilo  hivi karibuni nchini Afrika Kusini.


No comments:

Post a Comment

Pages