Na Victor Masangu,Kibaha
Halmashauri ya mji Kibaha kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 imekadiria kukusanya zaidi ya shilingi bilionj 45.8 kutokana na ruzuku, mapato yake ya ndani pamoja na mashirika mbali mbali ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kibaha Selina Wilson wakati wa kikao cha Baraza la madiwani kwa kipindi Cha robo ya tatu kuanzia mwezi januari hadi machi mwaka 2023.
Makamu huyo alibainisha kwamba kwa upande wa makusanyo kuanzia mwezi julai mwaka 2022 hadi machi 2023 wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 29.9 ikiwa sawa na kiwango cha asilimia 65.5.
Aliongeza kuwa halmashauri hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi julai 2022 hadi kufikia Machi 2023 kiasi cha shilingi mqilioni 587.8 ikiwa sawa na asilimia zipatazo 116 ya makisio ya mwaka.
Akizungumzia kuhusiana na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2022/2023 imepanga kutumia kiasi cha shilingi bilioni 113 kwa ajili kutumika katika miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira Hamis Shomari alisema kuwa kwa sasa zoezi la utambuzi wa wananchi waliovamia katika eneo la mtaa wa mkombozi limefanyika na kwamba wananchi 4509 tayari wameshatabuliwa.
"Uuzaji wa viwanja katika mtaa wa mkombozi umeshaanza ramsi tangu tarehe 24 mwaka huu ambapo wananchi walishajulishwa,ambapo jumla ya ankra ya viwanja 168 katika mtaa wa mkombozi zimeshatolewa,"alibainisha Shomari.
Akizungumzia kuhusiana na wananchi ambao wamevamia katika mtaa wa Lumumba tayari kazi ya utambuzi imeshafanyika ambapo wananchi wapatao 6952 wameshatambulika na kazi ya michoro 8 yenye viwanja 7,264 imekamilika.
Kwa upande wake Mwnyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba amewahimiza madiwani kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili iweze kuleta tija kwa maslahi ya wananchi.
No comments:
Post a Comment