HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 19, 2023

MWENGE WA UHURU WAMULIKA KIWANDA CHA TANBREED POULTRY LIMITED KUAGIZA WAWEKE MAZINGIRA SALAMA KWA WAFANYAKAZI WAKE

 Na Khadija, Kalili


KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru  Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amewataka viongozi  wa Kiwanda cha Tanbreed Poultry  Limited kuwajali wafanyakazi wake kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kazi na  kuwapa  vifaa vya kuwakinga  wasiweze kupata madhara wawapo kazini.



"Kiongozi huyo amesema hayo leo alipotembelea kiwandani hapo huku akiwangoza viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon   Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi  katika mbio za  mwenge  Wilayani hapa.


Amesema  hayo baada ya kutembelea Kiwanda hicho kinachomilikiwa  na kufanya biashara  sambamba na Kampuni  dada ya Interchick  Company Limited na Tanzania  Breeder and feed mill ambapo kiwanda hiki ni tawi  la Kiwanda  kilichopo Dar es Salaam ambapo pia kiwanda hiki kimeanza kufanya kazi  Aprili 2022.

Meneja  waKiwanda hicho cha Tanbreed  Poultry  Limited  Dickson

Gerald Malamsha ameahidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Kiongozi  wa mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa  Abdullah Shaib Kaim.


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon amesema kuwa kaulimbiu  ya mwenge wa Uhuru 2023  inasema 'Tunza  Mazingira  Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi  wa Viumbe  hai  kwa uchumi wa Taifa'.

Amesema hayo leo ikiwa ni kwenye mwendelezo wa mbio za Mwenge  Wilayani Kibaha Mkoani Pwani uliotembelea miradi mbalimbali Wilayani Kibaha.


Mwenge huo umepokelewa na 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Ali  Munde aliyepokea mwenge huo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kibaha  Vijijini Butamo Ndalahwa

 

"Sisi wananchi wa "Halmashauri ya Kibaha  Mji tunafuraha  kubwa  kuupokea Mwenge wa Uhuru"amesema Nickson.  "Halmashauri  ya Kibaha ina eneo la ukubwa  wa Km.750 sawa na ekari185,276.Kiutawala ina Tarafa 2,Kata14 na mitaa73,kwa mujibu  wa sensa ya  watu  na makazi ya mwaka 2022 kwa sasa  lwa pamoja tuungane katika 

kukabiliana na changamoto za dawa za kulevya kwa vijana wetu iliwemo kuwapa malezi bora na kuzingatia imani za dini mila na desturi zetu .

Wakati huohuo Kiongozi wa mbio za Mwenge  wa Uhuru Kitaifa Shaib amekagua mradi wa barabara ya Viwatilifu kwenye  kipande cha urefu wa Mita 400 kwa kiwango cha lami barabara  hiyo  inaanzia kwenye makutano ya barabara ya TAMCO hadi Mnarani (1.03 Km) na inapita katika eneo la  uwekezaji wa viwanda  manufaa ya mradi huu ni kuimarisha  maendeleo ya jamii na ukuaji wa uchumi" amesema Meneja wa TARURA Wilaya ya Kibaha  Samuel  Ndoveni.


Ndoveni amesema kuwa mradi huu umetekelezwa  na Mkandarasi M/S Mirogenia Investment CO.Limited  ya Jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Mil.496,755,000 kwa muda wa miezi sita ,mradi huu ulianza Septemba 2021 na ulitegemewa kukamilika Machi mwaka huu lakini kutokana na  mvua na  kuchelewa kwa msamaha  wa kodi (VAT exemption)kumesababisha kuongezeka  muda wa kumaliza  mradi  mpaka ifikapo Agosti  mwaka huu.


Amesema kuwa wamepata ushirikiano mkubwa wakati wa utekelezaji  wa mradi na wamepata ushirikiano mzuri kutoka  kwa viongozi  wa Mkoa wa Pwani,Wilaya, Halmashauri  na Kata katika kutatua changamoto mbalimbali  zilizojitokeza.

No comments:

Post a Comment

Pages