HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 18, 2023

KINANA AKUTANA NA RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNAM

  

 Leo, tarehe 18 mei 2023, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman O. Kinana ameongoza Ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo na Mhe. Vo Van Thuong, Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Jijini Ha Noi, Viet Nam.


Katika mazungumzo hayo, Ndg. Kinana aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, wa kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi  hizo mbili ili kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Vietnam.


No comments:

Post a Comment

Pages