HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2023

Rais Dk. Samia azidi kupongezwa

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga MNEC Ustadh  Rajab Abdulhaman Abdalah akikagua ujenzi wa daraja la Pangani.

Mhandisi wa Tanroad Eng Safia Maliki akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja la Pangani.


 

Na Mashaka Mhando, Pangani

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Tanga MNEC Ustadh Rajab Abdulhaman Abdalah, amesema wanaochukia sifa zinazotolewa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wafike katika miradi inayotekelezwa na serikali.

Akizungumza wakati akikagua ujenzi wa daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 ulioanza kujengwa, Mwenyekiti huyo wa chama, alisema katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Dkt Samia, ametoa fedha nyingi za miradi ya Maendeleo hapa nchini.

"Mara zote tunapompongeza na kumsifu mheshimiwa Rais wetu wengine huwa hawatuelewi na ili waelewe wafike site (eneo la mradi) waone anachokifanya kutekeleza ilani ya chama chetu," alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema Chama cha Mapinduzi wakati ule kikinadi ilani yake na kuanisha miradi mbalimbali wapinga Maendeleo ambao ni wapinzani walisema hayatawezekana jambo ambalo lilikuwa si kweli.

Awali akisoma utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo mradi unaotekelezwa na kampuni ya Ms Shandong Luqiua Group ya Kichina, Mhandisi wa Tanroad Mhandisi Safia Maliki Alisema mradi huo hadi kukamilika utachukua miezi 36 na utagharimu kiasi cha sh. 82,190,096,390.65.

Alisema serikali itaigharamia mradi huo kwa asilimia 11.16 na benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatoa fedha kwa asilimia 88.84.

Alisema mradi huo ulioanza Desemba mwaka jana na hadi kufikia mwezi huu utekelezaji wake umefikia asilimia 5 kwa kazi mbalimbali zimefanyika ikiwemo ujenzi wa daraja la muda katika daraja hilo.

Hata hivyo, alisema kuwa mradi unakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kusafirisha mitambo ng'ambo ya pili pamoja na wafanyakazi lazima walipe kwenye kivuko, uhamishaji wa nguzo za umeme, makaburi na miundombinu ya maji.

Mbunge wa Pangani na Waziri wa Maji Jumaa Hamidu Aweso, alisema daraja hilo likikamilika utakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Pangani katika kujenga uchumi wao.

Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa Mohamed, alisema moja ya mambo aliyoyafanya ni kuhakikisha wakandarasi wa barabara hiyo pamoja na daraja kuwapa kazi vijana wa Pangani.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Abdallah Mahmod alisema likatapokamilika daraja hilo wanaomba liitwe Awesso Bridge.

Mwenyekiti huyo aliridhishwa na utekelezaji wa mradi huo pamoja na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Tanga-Pangani hadi Bagamoyo.



No comments:

Post a Comment

Pages