Dar es Salaam — Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Magari Wilaya ya Kinondoni, Abdallah Rashid, amesema umoja huo ulianzishwa mwaka 2010 ukiwa na wanachama 520, huku idadi ya mafundi wa magari wilayani humo ikifikia 3,500.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa mbio za Mwenge katika eneo la Mbunju, alieleza kuwa umoja huo umekuwa na mchango mkubwa katika kuunganisha mafundi na kuboresha shughuli zao.
Katika tukio hilo, Mwenge wa Uhuru ulizindua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kinondoni, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma na kuinua uchumi wa wananchi.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Magari Wilaya ya Kinondoni, Abdallah Rashid, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mbio za Mwenge katika eneo la Mbunju jijinin Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Magari Wilaya ya Kinondoni, Abdallah Rashid.

.jpeg)





No comments:
Post a Comment