HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2023

Viongozi wa dini watema nyongo Kagera

 VIONGOZI WA DINI KAGERA WAMWANGUKIA RC MWASSA JUU YA MAADILI YA MATRAFFIC.


Na Mwandishi Wetu, Kagera


Baadhi ya Viongozi wa madhehebu ya dini Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi Fatma Mwassa kuona namna ya kuwarekebisha baadhi ya Maafisa Usalama Barabarani manispaa ya Bukoba ambao wameonekana  kutoonyesha maadili na heshima kwa Viongozi wa dini wanapokutana nao sehemu zao za kazi hasa pale wanapokuwa na dosari ndogo ndogo katika vyombo vyao vya moto.


Viongozi hao wametoa kauli hiyo wakati wakiongea katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mkoa wa Kagera.


Viongozi hao wa dini  wamesema kuwa licha ya wao kujitolea katika kazi hiyo ya kumtumikia Mwenyezi Mungu pengine hata bila malipo wamekuwa wakikutana na kadhia ya kutoheshimiwa na baadhi ya Maafisa hao wawapo Barabarani ambapo inapotokea wakawa na mapungufu kidogo katika magari yao wakati mwingine uombwa fedha na maafisa hao wakingali hawana fedha hizo kwa muda huo.


Akinukuliwa mmoja wa Viongozi hao amesema kuwa" 'Sisi hapa Mkuu wetu wa Mkoa unavyotuona tunajaribu kujitolea katika kazi hii ila Kuna wakati hata katika kazi hatupati hata posho iwe ni vikao au hata katika majukumu yetu ya kawaida ila changamoto kubwa hawa Ma Traffic wametufanya tukose heshima tunaomba waonywe wawe wanatupa muda wa kujipanga kwani muda huo tunakuwa hatuna fedha" alisema mmoja wa Viongozi hao wa dini.


Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi Fatma Mwassa amesema kuwa wakati wote maafisa hao wanahimizwa maadili Ila kwa maoni ya Viongozi hao ameelewa na kuona kuwa uwenda vijana hao wameenda nje ya utaratibu unaotakiwa.


RC Mwassa amesema  ni jambo baya kuona vijana wanaenda nje ya majukumu yao wakati wakijua majukumu yao yanawapasa kufanya nini.


"Nimewasikiliza bahati nzuri hapa Kuna Kaimu Kamanda wa Polisi hilo litafanyiwa kazi tutasimama ni lazima tuwapatie mafunzo na hasa mafunzo ya maadili" alisema Rc Fatma Mwassa.


Ameongeza kuwa itaandaliwa tume ya maadili ili iwapitishe katika Elimu hiyo kwa ajili ya kuwafanya wanatende kazi kwa mujibu wa sheria  kanuni na taratibu zilizopo ili kazi hiyo isigeuke kuwa kero.


Aidha Bi Fatma Mwassa ameongeza kuwa wataweka mitego itakayowabaini  maafisa hao wanaojihusisha na vitendo visivyofaa  ili waondolewe katika kazi hiyo na kupangiwa majukumu mengine.


Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema magari ya viongozi wa dini zamani yalikuwa yanatambulika kwa urahisi ila kwa sasa watumishi wamekuwa wengi  huku akiwaahidi  kuhakikisha anawanaondolea  changamoto hiyo kwani Serikali ipo kazini na kuwa ataifanyia kazi changamoto hiyo na kuwaomba watumishi hao wa Mungu kuona namna ya kuweka alama katika magari yao ili yatambulike na kuwaondoa katika changamoto hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages