Na Lydia Lugakila, Bukoba
Vijana Mkoani Kagera wanatarajia kujikwamua kiuchumi kupitia fursa ya ufugaji wa kisasa na wa kistaarabu utakaofanyika kupitia katika Ranchi za Serikali zilizopo Mkoani humo.
Kauli hiyo imebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi Fatma Mwassa katika kikao na Viongozi wa dini Manispaa ya Bukoba kilichofanyika katika ukumbi wa Mkoa huo.
Bi Fatma amesema Mkoa huo una Ranchi nyingi za Serikali ambazo watu wanaweza kufuga kisasa na kistaarabu na kuwa kwa sasa Ranchi nyingi kati ya hizo hazijaanza kutumika.
"Tutatengeneza vizuri utaratibu ili kutoa Fursa kwa Vijana kufuga Ng'ombe ili wanufaike na biashara hiyo hivyo ni jukumu letu Sisi kama Serikali kuwasaidia Vijana wapate mitaji ya Ng'ombe" alisema Bi Fatma.
Ameongeza kuwa changamoto iliyopo nikwamba bado Vijana hawajaandaliwa vizuri kuijua fursa hiyo Ila ana imani wataitambua fursa hiyo kwa haraka jambo litakalo saidia katika kuunyanyua Mkoa huo kuichumi.
No comments:
Post a Comment