HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2023

Zambia yaipongeza Tanzania kuboresha miundombinu ya Bandari

Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Serikali ya Zambia Mhe. Frank Tayali (Mb) ameipongeza Serikali ya Tanzania na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania - TPA kwa maboresho makubwa ya kimiundombinu yanayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akifungua Kongamano la Ushirikishwaji wa Wateja na Wadau wa Bandari ya Dar es Salaam, tarehe 31 Mei, 2023 Jijiji Lusaka, Zambia, Mhe. Tayali amesema maboresho yanayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam yanaongeza ufanisi katika utoaji wa Huduma Bandarini hapo na hivyo kufungua zaidi Biashara kati ya Tanzania na Zambia Pamoja na Nchi zisizo na Bahari zinazohudumiwa na Bandari ya Dar es Salaam.

Kangamano hilo limeandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia kwa lengo la kuwajulisha Wateja na Wadau wa Bandari kuhusu maboresho ya miundombinu katiia Bandari ya Dar es Salaam, Unafuu wa Tozo mbalimbali za Kibandari, kutambulisha huduma mpya za kibandari ikiwemo huduma ya kulipa tozo za Bandari Kidigitali pamoja na kupokea maoni na changamoto wanazokutana nazo Wateja na Wadau wanapotumia huduma za Bandari na kuanzia Bandarini hadi Mpakani.

Kongamano hili limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji nchini Zambia Mha. Frederick Mwalusaka, Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Jenerali Mathew Mkingule, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mha. Juma Kijavara, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA Dkt. George Fasha, Maafisa wa Masoko na Uhusiano wa TPA kutoka Makao makuu na Ofisi ya TPA nchini Zambia, Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, Wadau wengine wa Huduma za Bandari wa Tanzania pamoja na Wateja na Wadau wa Bandari ya Dar es Salaam nchini Zambia.



No comments:

Post a Comment

Pages