Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA), Mhandisi Kassim Ali Omar (katikati) akiwa na watendaji wengine katika ziara ya kutembelea miradi ya kimaendeleo yainayosimamiwa na ZBA.
Na Sabiha Keis (WAMM)
MKURUGENZI Mkuu Wakala wa Majengo Mhandisi Kassim Ali Omar amesema kuwa
mashirikiano ya kiutendaji baina ya Wakala wa Mjengo Zanzibar(ZBA) na Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) utaziwezesha Taasisi hizo mbili kuweza kufanya kazi kwa
ufanisi zaidi kwa vile majukumu yake yanalingana.
Alifahamisha kuwa ziara hiyo ya watendaji kutoka Wakala wa Majengo Tanzania ni
moja ya maagizo ya viongozi wa nchi kuzitaka taasisi zinazofanana
majukumu yake kushirikiana pamoja kiutendaji ambapo kwa sasa Taasisi hizo mbili
zina mpango wa kutengeneza hati ya makubaliano(Mou)baina yao.
“ziara hii inalenga zaidi mashirikiano ya kiutendaji kwa taasisi mbili hizi na
tayari tumeshafanya kikao ili tuweze kutengeneza hati ya makubaliano na tuweze
kufanyakazi kwa karibu sana”alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) Mhandisi Loishorwa Likimaitare ameipongeza Taasisi ya Wakala wa Majengo(ZBA)kwa namna
wanavojitahidi katika kutekeleza kazi zake za usimamizi wa miradi
ingawa kumekuwa na uhaba wa watendaji kulingana na wingi wa kazi zilizopo
hivyo ameiomba Serikali kuwaongezea watenadaji hao ili waweze kufanyakazi
kwa ubora na kukamilisha miradi wanayosimamia kwa wakati.
Tumefarijika sana kuja kuona kazi ambazo zinatekelezwa na wenzetu hawa na
tumejifunza mengi kutoka kwao na hatua ya miradi wanayoisimamia kwa kweli
inaridhisha hivyo nawaomba waongeze kasi ya uajibikaji ili Serikali iweze
kuendelea kuwaamini”alisema Mkurugenzi huyo.
Nae Mhandisi Mohammed Nahoda Mohammed kutoka Wakala wa Majengo Zanzabar
amefahamisha kuwa kwa Wakala inetekeleza miradi mbali mbali ikiwemo miradi ya
ofisi ya uhamiaji ya Mkoa wa Mjini Magharib , mradi wa Shirika la Nyumba
kwamchina na masoko matatu ya Chuini pamoja na Jumbi.
Aidha ameziomba taasisi mbali mbali za Serikali kuwatumia wakala wa majengo kwa
vile taasisi hiyo ndio ipo kisheria na imepewa dhamana ya usimamizi wa miradi
mingi ikiwemo ya Serikali na wamekuwa wakifanyakazi kwa kwa kiwango
kinachokubalika nchini.
Akizungumzia kuhisiana na Ziara hiyo Mhandisi Daniel Mwakasungula kutoka Wakala
wa Majengo Tanzania amefahamisha kuwa ziara hiyo ni miongoni mwa maagizo ya
viongozi wa nchi kutaka Taasisi zinazolingana kimajukumu kuweza kushrikiana
pamoja ili kuweza kupiga hatua za kimaendeleo nchini.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja ofisi ya jeshi la uhamiaji mazizini,jengo la
wakala wa chakula dawa na vipodozi,mradi wa ujenzi wa nyumba kwamchina,mradi wa
soko la Mwanakwerekwe pamoja na Soko la Jumbi.
No comments:
Post a Comment