HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2023

BODI YA LIGI 'TPLB' YAWAMWAGIA MAUA WADAU WA SOKA


Na John Richard Marwa 


BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewamwagia Maua wadau mbalimbali wa mpira wa miguu kwa kufanikisha kumalizika kwa msimu wa Ligi 2022/2023 kwa ubora mkubwa wa usimamizi na 

uendeshaji wa michezo yote ya Ligi Kuu ya NBC, Ligi ya Championship na First League.


Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi kupitia mitandao ya kijamii asubui ya leo ikikiri kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau wake wote.


"Katika kufanikisha hilo, Bodi inakiri na kushukuru kupata ushirikiano 

mkubwa kutoka kwa wadau wake wote wakiongozwa na mdau mkuu, 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais

wetu mpendwa, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.



"Pamoja na kurahisisha masuala mengine ya kiuendeshaji na usimamizi waLigi, Serikali imetengeneza mazingira bora na salama kwa michezo ya Ligi kuchezwa nchini huku klabu zetu zikisafiri kutoka sehemu moja 

kwenda nyingine bila vikwazo wala changamoto za kiusalama au 

miundombinu.



"Ushauri na miongozo bora kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) 

imekuwa ikiongeza ubora katika usimamizi na uendeshajiwa Ligi, jambo linalochochea ukuaji wa Ligi zetu kwa kushirikiana na klabu ambazo zimekuwa zikifanya kazi kubwa katika kuboresha timu zao." Imeeleza taarifa hiyo na kubainisha kuwa.



"Bodi inawashukuru kwa dhati wadhamini wa LigiKuuwakiongozwa na 

mdhamini mkuu, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga, Azam Media Ltd na mdhamini mwenye haki za matangazo ya Redio, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).



"Uwepo wa wadhamini hawa umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto za kifedha kwa klabu zetu jambo lililoongeza hali ya ushindani viwanjani.



"Bodi inafahamu umuhimu mkubwa wa mashabiki wa klabu zetu hivyo 

licha ya kuwashukuru sana kwa kuziunga mkono klabu hizo katika msimu wa 2022/2023, inawasihi waendelee kuhamasishana kuhudhuria kwa wingi viwanjani kwenye msimu wa 2023/2024 ili kuzishangilia timu zao

zikicheza michezo ya Ligi." Taarifa hiyo imeongeza kuwa.



"Ubora wa Ligi zetu umeendelea kutajwa ndani na nje ya nchi kwa sababu Wanahabari na vyombo vya Habari. nchini wameendelea kufanya kazi kubwa na bora ya kutangaza mazuri ya Ligi zetu ikiwa ni pamoja na kukosoa ama kutoa ushauri wenye malengo ya kuboresha zaidi Ligi.


"Bodi inawashukuru sana ikiwa na matumaini kuwa wataendelea kushirikiana nayo katika msimu wa 2023/2024.



"Bodi ya Ligi inavishukuru vyama vya mpira wa miguu vya mikoa (RFAs) kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika masuala ya kiundeshaji 

na usimamizi wa Ligi hasa maandalizi ya michezo ya Ligi.



"Shukrani za dhati pia ziende kwa vyama vishiriki,Chama cha Waamuzi (FRAT), Chama cha Madaktari (TASMA), Chama cha Makocha (TAFCA), Chama cha 

Wachezaji Mpira wa Miguu (SPUTANZA) na Chama cha Sokala Wanawake (TWFA) kwa kuendelea kuiunga mkono Bodi katika utekelezaji wa majukumu yake." Imesema taarifa hiyo.


Katika hatua nyingine taarifa imeeleza kuwa Bodi inaendelea na maandalizi ya msimu wa 2023/2024 ambapo ushirikiano wa wadau tajwa hapo juu utakuwa na mchango mkubwa katika kutimiza lengo la kupata msimu bora zaidi.


No comments:

Post a Comment

Pages