HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 25, 2023

KLABU ZAKUMBUSHWA KUBORESHA VIWANJA KUELEKEA MSIMU WA 2023/2024

 Na John Marwa


KLABU za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL, Ligi ya Championship na Ligi Daraja la kwanza, zimekumbushwa kuboresha viwanja kw ajili ya kuongea ubora wa Ligi msimu ujao.



Hayo yamebainishwa na Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu ya NBC PL, Karim Boimanda kupitia kipindi cha U Live cha Uhai FM jioni ya leo.


Boimanda amesema kumalizika kwa msimu huu ni maandalizi ya kuelekea msimu ujao wa 2023/24 kwa Ligi zote.


"Kumalizika kwa msimu huu ambao umekuwa msimu bora sana ni kishiria cha maandalizi ya kuelekea msimu ujao ambao tunataraji kuwa utakuwa msimu bora zaidi kuliko msimu uliomalizika.


"Nitoe wito kwa klabu. zetu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC PL, Championship na Ligi Daraja la kwanza kuhakikisha kuwa wanaboresha viwanja Ili tuweze kuwa na msimu bora zaidi wa 2023/24.


"Ukitazama viwanja ambavyo tumekuwa navyo msimu huu ni wazi kila mmoja wetu atakili kuwa Ligi yetu imechezwa kwenye viwanja bora kuliko misimu iliyopita.


"Matumaini yetu ni kuwa na Ligi bora zaidi kwa msimu ujao, kama Bodi ya Ligi tunaamini tunaweza kuwa na viwanja bora zaidi kuliko vilivyopo sasa, hivyo ni jukumu la kila mdau ni kuhakikisha anatoa mchango wake kwa ajili ya mpira wetu." Amesema Boimanda.


Boimanda amewashukuru wadau wote kwa mchango wao walioutoa na kuifanya msimu uliomalizika kuwa msimu bora ndani ya Uwanja na nje ya Uwanja.

No comments:

Post a Comment

Pages