HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2023

CPS: Kubadilisha mandhari za makazi Afrika Mashariki

Mkurugenzi Mtendaji wa CPS Sebastian Dietzold (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi mpya ya Kampuni ya CPS zilizopo Oyster Bay jijini Dar es Salaam.

Graham Leslie akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘The Soul Fumba", ina nyumba 200 za aina yake kwa ajili ya wasafiri, zilizojengwa kimkakati Magharibi ya Pwani ya Mji wa Fumba.
Abdulrahman Said akizungumzia mradi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing, Fred Msemwa (katikati) akizungumzia faida za mradi huo.
Kampuni ya  CPS inayojishughulisha na ujenzi nchini Tanzania, imezindua mradi wake mpya wa ‘The Soul Fumba’ uliopo katika mji wa kisasa wa Fumba Town-Nyamanzi mjini Zanzibar.

 

Kufuatia mafanikio makubwa ya mradi wake mwengine unaojulikana kama ‘The Soul’ uliopo Paje Zanzibar ambapo nyumba zote ziliuzwa mapema mwaka huu, CPS imeamua kutanua wigo wake kwa kuimarisha pwani ya Afrika Mashariki kwa miji ya kisasa inayozingatia mandhari na haiba rafiki kwa mazingira.


Akiongoza uzinduzi wa Ofisi mpya za kampuni hiyo zilizoko Masaki jijini Dar Es Salaam, karibu na Kaffe Koffee, Mkurugenzi Mtendaji wa CPS Sebastian Dietzold alitambulisha mradi huo mpya wa ‘The Soul Fumba,’ kwa fahari kubwa huku akibainisha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika shughuli mbalimbali za utendaji wa CPS.


Sanjari, Bw. Dietzold alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Serikali ya Zanzibar, kwa kuiunga mkono kampuni hiyo na kuchochea mafanikio yaliyopatikana na kampuni hiyo.


"The Soul Fumba" ina nyumba 200 za aina yake kwa ajili ya wasafiri, zilizojengwa kimkakati katika upande wa magharibi ya pwani ya mji wa Fumba na miundombinu murua, ikijivunia huduma mbalimbali kama vile vituo vya afya, viwanja vya michezo, bustani zilizotayarishwa na kuendelezwa kwa ustadi na taaluma ya permaculture, maeneo ya biashara za rejareja, maeneo ya chakula na vinywaji, na maeneo ya ofisi. Uwepo wake karibu na Mji Mkongwe na uwanja wa ndege huhakikisha urahisi wa kufikika na utulivu kwa wakaazi na wageni.


Zaidi ya hayo, "The Soul Fumba" inatoa fursa kwa faida kubwa katika uwekezaji kwa kunufaika na sekta ya utalii inayostawi Zanzibar na thamani inayotokana na kukua kwa kasi kwa miji. Hii  inafanya "The Soul Fumba", kuwa chaguo bora lililo sahihi kwa wote: wawekezaji na watu wa aina zote: wapenzi, wanandoa, na familia zinazotafuta makazi barani Afrika.


Ikiwa katika sehemu muhimu ya Mradi wa Fumba katika Eneo Huru la Kiuchumi, "The Soul Fumba" inakaribisha wanunuzi kutoka nje ya nchi.


Aidha, motisha za kuvutia zimetangazwa na Serikali ya Zanzibar, zikiwemo viza za ukaazi kwa uwekezaji wa kuanzia dola 100,000 na mafao/msamaha wa kodi. CPS imedhamiria kuweka mazingira ya kukaribisha wawekezaji wa kimataifa wanaopenda soko la mali zisizohamishika la Zanzibar.


Nyumba za "The Soul Fumba" zinauzwa katika mfumo wa off-plan, hivyo kuruhusu wanunuzi kumiliki nyumba hizo kwa malipo ya awali ya 15%. Mpango wa malipo wa miaka 5 unapatikana, na malipo ya kila mwezi yanaanzia $1,270. Afisa Mkuu wa Biashara wa CPS, Tobias Dietzold, anaeleza kwamba wanunuzi wanapolipa, nyumba zao zitatayarishwa kwa ajili yao ili kuwawezesha kuhamia, kuhakikisha matumizi ya kawaida na rahisi.


Kila mnunuzi katika mradi wa "The Soul Fumba" atapokea hati miliki kwa miaka 99, ikiwapa haki ya kurithi, kuweka rehani, kuuza na kukodisha mali yao. CPS imejidhatiti kuhakikisha thamani ya muda mrefu na usalama kwa wanunuzi, kuwaruhusu kutumia vyema uwekezaji wao.


Uzinduzi wa "The Soul Fumba" uliambatana na mjadala ulioshirikisha watu mashuhuri, akiwemo Graham Leslie, Mwenyekiti Mtendaji wa The Hotel Association Zanzibar & President of Conservation Capital; Fred Msemwa, Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Investment; na Abdulrahman Said, Mshirika Mkuu wa Bankable. Jopo hilo lililenga kuelezea fursa zilizopo katika sekta ya mali isiyohamishika inayochochewa na sekta ya utalii inayostawi kwa kasi.


Hivi majuzi Zanzibar imejinyakulia hadhi ya kuwa kivutio kikuu cha utalii barani Afrika, kama ilivyotangazwa na chapisho la "The Travel Magazine." Ikiyapiku maeneo mashuhuri kama vile Mlima Kilimanjaro, Cape Town, na Masai Mara ya Kenya, sekta ya utalii ya Zanzibar sio tu imeongezeka hadi kufikia viwango vya kabla ya janga la ugonjwa lakini pia inatarajia ukuaji wa 30% ikilinganishwa na 2022. Uchumi unaostawi wa nchi unatarajiwa kukua kwa zaidi ya 7% mnamo 2023.


Kwa kuwa na Serikali inayokaribisha uwekezaji kutoka nje, sekta ya majengo Zanzibar imepata ukuaji wa haraka katika miaka ya hivi karibuni na kuifanya Zanzibar kuwa uwanja mzuri wa ukuaji na upanuzi, na fursa zisizo na mwisho kwa wale walio na changamoto.


CPS inawaalika wanunuzi na wawekezaji watarajiwa kujipatia fursa adhimu iliyotolewa na "The Soul Fumba" na wajiunge na safari ya kuunda jamii murua katika Mji wa Fumba. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya CPS au wasiliana na timu yao ya mauzo.

No comments:

Post a Comment

Pages