HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 07, 2023

Huduma kidigitali zaongeza mapato TRA, kukusanya trilioni 23.1


Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanznia (TRA), Richard Kayombo, akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na mamlaka hiyo kwa waandishi wa habari ambao ni wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC).
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.


Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hamad Mterry akitoa mada.

  

Afisa Mwandamizi Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Julieth Kidemi, akitoa mada katika semina hiyo.


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema utoaji  wa huduma kwa njia ya kidigitali umeimarisha na kuongeza mapato kwa kiasi kikubwa ikiwamo kufikia malengo ya ukusanyaji kodi kwa mwaka wa fedha 2022/2023.


Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa Kodi, Richard Kayombo wakati akifungua mafunzo ya waandishi wa Chama cha Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) kuhusu ukusanyaji wa kodi kwamba mfumo wa digitali umesaidia kupunguza msongamano kwa wafanyabisahara kufika ofisini.

 
"Mfumo wa kidijitali  kwa sasa TRA imerahisisha upatikanaji wa hudumu kwa wanyabiashara hususani kwenye suala la namba ya mlipakodi  (TIN namba), katika mfumo mzima wa forodha mfumo huo unarahisisha huduma, ikaleta uwazi, uwajibikaji na kuongeza ufanisi," alisema Kayombo.
 

Alisema lengo la TRA kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ni, kufikia  Trillion 23.1 na kwamba mpaka kufikia June 30,  malengo yaliyopangwa  yatakuwa yamefikiwa, kwa kuwa  ulipaji wa kodi Kwa wafanyabiashara ni kunasaidia kuongeza  maendeleo ya nchi.

 
"Kuna tofauti kubwa katika miaka 10 iliyopita na Dar es Salaam ya sasa ni, taa kila  mahali unapopita kuna mabadiliko na hayo yote yanatokana na ulipwaji wa kodi , ikilipwa vizuri, tunatoa fedha kwa serikali kwa ajili ya kutengeneza miundombinu mbali mbali,"alisema Kayombo.

 
Alisema ili kizuia upotevu wa mapato kwa wanaotumia njia mbali mbali ikiwepo bandari bubu TRA ina mpango madhubuti wa kuanzisha kikosi cha kudhibiti magendo kwa mipaka yote ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Pages