HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 09, 2023

'Kampuni nyingi hazijawasilisha wamiliki manufaa'

Exuperius Kachenje


Exuperius Kachenje

Wakala wa Usajili wa Kampuni na majina ya biashara nchini (Brela) imesema kampuni nyingi hazijatimiza matakwa ya kisheria ya kuwasilisha taarifa za Wamiliki Manufaa na kwamba kutofanya hivyo kunaaaweka hatarini kulipa faini inayofikia shilingi milioni 10.

 

Akizungumza katika semina ya Wahariri wa vyombo vya habari jana, Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara, Medard Rweyemamu alisema hitaji la kuongeza uwazi kwenye kampuni ni la kisheria hivyo linapaswa kutekelezwa.

Alibainisha kuwa tangu kupitishwa kwa kanuni za sheria hiyo mwaka 2022 kampuni  20,000 pekee zimetimiza agizo hilo la kisheria lakini idadi kubwa hazijatimiza wajibu huo.

"Kuandikisha Wamiliki Manufaa ni jukmu la kampuni,  kampuni zote lazima ziwe na oradha ya  Umiliki Manufaa, taarifa zao zote lazima ziwepo na ziwasilishwe Brela na zisizotimiza takwa hilo zitalipa faini  ya Shilingi milioni tano hadi kumi,"alisema Rweyemamu.

Awali, akifungua semina hiyo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, aliyekuwa mgeni rasmi alizishauri kampuni zilizosajiliwa na Brela, kuwasilisha taarifa zao za umiliki manufaa ili kuisaidia taasisi hiyo kuboresha matakwa ya kisheria na kuepuka faini akieleza kwamba kampuni nyingi hazijawasilisha taarifa hizo.

"Sheria ya Brela sura  namba  212 inaeleza wazi kuhusu upatikanaji wa taarifa za wamiliki manufaa, kanuni za sheria hiyo zimepitishwa mwaka jana 2022 na waziri husika, lakini bado kampuni nyingi hazijawasilisha taarifa zao kuhusu umilikii manufaa. Kampuni zitambue, kuna faini ya shilingi milioni tano hadi milioni kumi,"alisema.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji wa Brela, Andrew Mkapa aliyezungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Brela, Godfrey Nyaisa, alisema Brela inafanya kazi kwa karibu na Brela katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kwa wakati na kwamba baada ya sheria kupitishwa na kanuni kutungwa, Brela imeona kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu Umiliki Manufaa.

No comments:

Post a Comment

Pages