HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 08, 2023

Waliojiunga na CCM, wasifu utekelezaji wa ilani


 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ustadh Rajabu Abdalahman Abdalah MNEC akizungumza na wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji Jumaa Hamidu Awesso akizungumza katika mikutano mjini Pangani katika ziara ya Mwenyekiti.

 

Na Mashaka Mhando, Tanga


WANACHAMA wapya waliorejea Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Tanga, wameeleza kuridhishwa kwao na utekelezaji wa ilani ya chama kwa kazi mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Wakizungumza katika mikutano mbalimbali ambayo mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ustadh Rajabu Abdalahman Abdalah (MNEC), walisema Maendeleo yanayoletwa na Rais katika maeneo mbalimbali hawana budi kumuunga mkono.


Haji Rashid Nundu aliyekuwa Chama cha Wananchi (CUF) wilayani Pangani, alisema Rais, Mbunge wa Pangani Jumaa Awesso, Mwenyekiti wa CCM mkoa, wamemvuta kujiunga na CCM baada ya kuona miradi mbalimbali inavyotekelezwa katika wilaya hiyo.

"Rais ametupa Waziri wa Maji kijana wetu Awesso (Jumaa Hamidu) Maendeleo hapa Pangani tunayaona shule za jengwa, hospital zajengwa, barabara za jengwa haya mimi nabaki upinzani kwanini?" Alisema Nundu ambaye ni kaka wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tanga marehemu Omari Nundu.

Alisema hata hamasa na ufuatiliaji wa ilani ya CCM unafanywa na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ustadh Rajabu katika ziara zake anazofabya mkoa mzima, zimemvuta kujiunga na CCM kwasababu ni Mwenyekiti wa aina yake kutokea mkoani Tanga hajawahi kumuona Mwenyekiti anafanya ziara na kukaa siku tatu kila wilaya.

"Lakini mnyonge mnyonge Rais wetu anaupiga mwingi, amefungua nchi lakini pia ameleta fedha tunaona daraja linajengwa hapa Pangani," alisema Nundu.

Mwanachama mwingine Abdulhaman Hassain Omari aliyekuwa vyama vya CUF na ACT-Wazalendo katika Jiji la Tanga, alisema kuna fikra mbaya imejengeka kwamba ukitoka upinzani kujiunga na CCM umehongwa, si kweli.

"Tukitoka upinzani kuha CCM unaambiwa umehongwa si kweli ndugu zangu, mbona ukitoka CCM ukienda upinzani huambiwi umehongwa?" Alisema Abdalahman ambaye amewahi kuwa diwani kata ya Msambweni vipindi viwili.

Alisema kazi zinazofanywa na serikali kupitia rais Samia hazina mfano mpinzani kubaki kwenye vyama hivyo ni kujitafutia ugonjwa wa moyo.

Akizungumza katika mikutano mbalimbali Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ustadh Rajabu aliwataka wana-CCM kuacha kuwatukana wapinzani na badala yake wanapokuwa kwenye mikutano y hadhara waeleze kazi nzuri zilizofanywa na serikali.

Alisema matusi na kejeli waachiwe wapinzani kwasababu hawana ya kusema kwakuwa CCM imeweza kutekeleza yale yaliyonadiwa kwenye ilani mwaka 2020 wakati wakiomba kura kwa wananchi.

Alisema katika mkoa wa Tanga rais Dkt Samia ameweza kutoa kiasi cha sh 95,405,488,719 kwa ajili ya sekta ya elimu na afya alileta kiasi cha sh 83,542,389,222 kwa kipindi tangu awe Rais miaka miwili iliyopita.

"Ndugu zangu tumuunge mkono rais ifikapo 2025 mkoa wetu wa Tanga uwe wa kwanza kwa kumpa kura nyingi," alisema Mwenyekiti huyo.

Katibu wa CCM mkoa wa Tanga Suleiman Mzee Suleiman, alisema katika wilaya nne ambazo Mwenyekiti amezitembelea jumla ya wanachama wapya 480 wamejiunga na CCM.


No comments:

Post a Comment

Pages