HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 28, 2023

KAMPUNI YA RISS AND SONS INDUSTRIES YA CONGO YATIMIZA MIAKA 30

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Riss and Sons Industries (RSI), Ambroise Basizi, akizungumza katika Maonyesho ya Kibiashara, Kilimo Uwekezaji na Utalii ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya CCM Manispaa ya Bukoba.

Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa.


Na Lydia Lugakila, Bukoba



Kampuni ya uzalishaji wa vinjwaji kutoka Bukavu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetimiza miaka 30 huku Mkurugenzi wa kampuni hiyo akitaja mafanikio yaliyopatikana kwa wa raia wa Congo Burundi Rwanda na Tanzania.

 Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ambroise Basizi Risasi amejivunia mafanikio ya kuwafikia raia wa Congo, Burundi, Rwanda na Tanzania kutokana na kuzalisha kinywaji kiitwacho Ngai Ngai kinachotengezwa kwa rosela baada ya kuwasaidia watumiaji katika kuondokana na matatizo ikiwemo ugonjwa wa Presha na kuongeza Vitamin C.

Akiizungumzia Kampuni hiyo Ambrose ambaye ni raia kutoka nchini Congo ambaye kwa sasa yuko mkoani Kagera kwa ajili ya maonyesho ya kibiashara, kilimo uwekezaji na utalii ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya CCM Manispaa ya Bukoba mkoani humo.


Amesema kuwa maonesho hayo yamemsaidia kwani amepata kutambulisha biashara yake na kuongeza elimu kwani ni mara yake ya kwanza kufika Mkoani humo ambapo pia amekipanga kuboresha zaidi kinywaji hicho ili kuuza katika mataifa mengine.

Kampuni yake ya Riss and Sons Industries ilianzishwa mnamo mwaka 1993, ambapo Mkurugenzi huyo ameeleza kufurahishwa na hali ya kibiashara ya Mkoani Kagera, hali ya hewa ikiwemo namna alivyopokelewana waandaaji wa maonyesho hayo.

Aidha Mkurugenzi huyo aliitaja changamoto anayokumbana nayo kuwa ni pamoja na uhaba wa upatikanaji wa chupa za kuhifadhia kinywaji hicho.

Hata hivyo ikumbuke kuwa Nchi mbali mbali ikiwemo Congo, Uganda wapo Mkoani Kagera katika Maonyesho ya kibiashara, kilimo, uwekezaji, na utalii yaliyoandaliwa ikiwa ni kuunga mkono juhudi za kuukomboa Mkoa huo kiuchumi huku yakibeba kauli mbiu isemayo" WEKEZA MKOA WA KAGERA KWA MAENDELEO YA TAIFA.

No comments:

Post a Comment

Pages