HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 28, 2023

𝗝𝗘𝗭𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗞𝗨𝗗𝗘 𝗬𝗔𝗦𝗧𝗔𝗔𝗙𝗜𝗦𝗛𝗪𝗔 𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔

Na Mwandishi Wetu 


Klabu ya Simba imestaafisha jezi namba 20 iliyokuwa ikivaliwa na aliyekuwa kiungo wa wekundu hao wa Msimbazi Simba Jonas Gerald Mkude 'NunguNungu Master'



Uamuzi huo ni sehemu ya heshima ambayo Simba imeamua kumpa nyota huyo baada ya kuitumikia klabu kwa miaka 13


Mkude ambaye alitokea kwenye shule ya vijana ya Simba na kudumu katika kikosi cha wakubwa kwa takribani miaka 13 ameondoka katika klabu hiyo baada ya mkataba wake kufikia ukomo msimu uliomalizika.


Jezi namba 20 haitakuwepo msimu ujao hadi pale atakapopatikana muhitimu mwingine mwenye kuakisi kile ambacho Mkude amefanya klabuni hapo


Aidha klabu hiyo imepanga kumfanyia makubwa Mkude ikiwa ni kuagwa kwa heshima siku ya Simba Day 2023 huku ikimpa nafasi ya kurejea klabuni hapo baada ya maisha ya kucheza mpira kama ilivyo kwa Musa Hassan Mgosi na Ma Legend wengine wa klabu hiyo.


Akizungumza juu ya hilo Meneja Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema Mkude kama Simba wataendelea kumuenzi Mkude kama mchezaji mahiri na wakukumbukwa katika mitaa ya Simba.


"Tutaenda kumuaga Mkude kwa heshima yake anayostahilia. Katika Simba Day kama wanasimba tutamuaga kwa ukubwa anaostahili. Mashabiki watamuaga, timu zetu  za vijana zitamuaga na timu yetu ya msimu ujao nao watamuaga Mkude.


"Mkude ni Simba na ataendelea kubaki Simba katika maisha yake yote. Akimaliza kucheza mpira nafasi yake hapa Simba ipo aidha kama Kocha ama kiongozi ndani ya Simba." Amesema Ahmed.

No comments:

Post a Comment

Pages