HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2023

TANZANIA YAPANDA VIWANGO FIFA

Na Mwandishi Wetu

Kwa mara ya kwanza baada ya takribani mwaka mmoja, Tanzania imepanda kwenye viwango vya ubora vya FIFA.

Kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya ubora ya FIFA iliyotolewa leo, Juni 29, Tanzania imepanda kwa nafasi 6, kutoka nafasi ya 130 hadi nafasi ya 123.

Mara ya mwisho Tanzania kupanda viwango ilikuwa Agosti 25, 2022 pale ilipotoka nafasi ya 131 hadi ya 130. Baada ya hapo Tanzania ilifunga ndoa na nafasi ya 130 hadi ndoa hiyo ilipovunjika leo.

FIFA hutoa viwango vya ubora kwa wanachama wake kila baada ya miezi mitatu. Kabla ya leo, mara ya mwisho ilikuwa Aprili 6, 2023.

Kupanda kwa viwango kwa Tanzania kumetokana na kuongezeka kwa alama zake kutoka 1125.89 kwenye ripoti ya mara ya mwisho hadi 1138.79 kwenye ripoti ya sasa.

CECAFA 1. Uganda (Afrika 19, duniani 92) 2. Kenya (Afrika 22, duniani 105) 3. Tanzania (Afrika 32, duniani 123) 4. Sudan (Afrika 39, duniani 131) 5  Burundi (Afrika 41, duniani 140)

AFRICA 1. Morocco (duniani 13) 2. Senegal (duniani 18) 3. Tunisia (duniani 31) 4. Algeria (duniani 33) 5. Misri (duniani 34)


DUNIANI 1. Argentina 2. Ufaransa 3. Brazil 4. England 5. Ubelgiji



No comments:

Post a Comment

Pages