HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2023

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA JULAI MOSI, MOTO UTAWAKA

Na John Marwa


DIRISHA la usajili majira ya joto kuelekea msimu mpya wa 2023/24 utafunguliwa kesho Julai mosi, huku dirisha dogo likitarajiwa kufunguliwa Desemba 16.



Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeeleza kuwa dirisha litafunguliwa Julai Mosi na kufungwa Agosti 31.     


"Dirisha la usajili (FIFA Connect) kwa klabu za Ligi Kuu ya NBC (NBC PL), Championship League (CL), First League (FL) na Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2023/24 unnafunguliwa Juali 1, na kufungwa Agosti 31, 2023.   Klabu zinatakiwa kufanya usajili na uhamisho wa wachezaji.  


"Hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili, tafadhali zingatia muda huu wa usajili na uhamisho. Kwa changamoto yoyote wasiliana na idara ya Mashindano ya TFF.           


"Usajili wa uhamisho wa wachezaji kwa dirisha dogo utafunguliwa Desemba 16 na kufungwa januari 15, 2024." Imeeleza taarifa hiyo.


No comments:

Post a Comment

Pages