HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 23, 2023

TRA 'yaliota' jeshi usu

 
-Yawaita wenye vitambulisho vya ujasiriamali


Exuperius Kachenje


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA),  inafikiria kuwa na jeshi usu katika majukumu yake kukabiliana na magendo na ukwepaji kodi.


 TRA pia imewataka wafanyabiashara wote wenye vitambulisho vya mjasiriamali kujisajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN), lakini hawatalipa kodi huku ikieleza kuwa kutokuwa namba ya TIN ni kosa la jinai.  


Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amebainisha hayo jijini Dar es Salaam juzi, akibainisha kuwa moja ya mianya mikubwa inayopoteza mapato nchini na kuhatarisha maisha ya wananchi wa Tanzania ni magendo. 


Alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari hizi kwenye mahojiano, nje ya ukumbi wa semina katika Chuo Cha Kodi Dar es Salaam, ambapo wanahabari wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam(DCPC), walipewa elimu kuhusu kodi, juzi.


"Wazo la kuwa na utaratibu kama wa kijeshi lipo, japo bado linafanyiwa kazi, likiruhusiwa litakuwa jema kwa sababu sio tu tutadhibiti mapato, bali pia tutashirikiana na vyombo vingine kuimarisha ulinzi wa taifa letu,” alisema Kayombo. 


Kwa mujibu wa Kayombo, mianya na vipenyo vya kupitisha magendo,vinalikosesha mapato taifa, pia vinahatarisha afya   na usalama wa wananchi kwani bidhaa zinazopitishwa huwa hazikufanyiwa vipimo kubaini ubora wake, hivyo ni hatari kwa wananchi kulishwa vyakula visivyofaa vinayoweza kugharimu maisha ya watanzania.


Akizungumzia kuhusu namba za utambulisho wa mlipa kodi maarufu Namba za TIN, Kayombo alisema sheria ya TRA sasa inaeleza wazi kuwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea lazima asajiliwe kama mlipakodi na kupewa namba ya utambulisho (Namba ya TIN).


“Kisheria ikifika Desemba mwaka huu 2023 kama una miaka 18 na kuendelea au  mfanyabiashara mwenye kitambulisho cha mjasiriamali na huna namba ya TIN ni kosa kisheria. Kukosa namba ya TIN ni kosa la jinai,” alisema Kayombo.


Alifafanua kuwa sheria inawataka wenye vitambulisho vya ujasiriamali kuwa na namba za TIN, lakini hawatalipa kodi kutokana na kiwango wa mitaji yao kuwa cha chini.
Awali, Kaimu Meneja kwa Mlipakodi wa TRA, Hemed Mterry alisema kodi ni jukumu la kisheria ambapo hukusanywa kwenye kipato.

No comments:

Post a Comment

Pages