HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 10, 2023

Wanawake KKKT Ushirka wa Boko Wametoa Msaada kwa Watoto Muhimbili

Mchungaji Msaidizi Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boko, Musa Nathaniel (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya matibabu Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Redemptha Matindi, kwa ajili ya watoto wanaopata matibabu ya saratani hospitalini hapo. Vifaa hivyo vimetolewa na Umoja wa Wanawake wa Kanisa la KKKT Usharika wa Boko.


Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Redemptha Matindi, kabla ya kupokea msaada wa vifaa vya matibabu kutoka kwa Wanawake wa KKKT Usharika wa Boko ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Kanisa la KKKT Usharika wa Boko, Mary Lema, akizungumza wakati wa matendo ya huruma na kukabidhiano ya vifaa vya matibabu kwa uongozi wa Hosptitali ya Taifa Muhimbili. 

Mchungaj Msaidizi Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boko, Musa Nathaniel, akizungumza wakati wa matendo ya huruma na kukabidhi vifaa vya matibabu kwa uongozi wa Hosptitali ya Taifa Muhimbili. 


NA JOHN MARWA

 

UMOJA wa Wanawake Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boko wametoa msaada wa vifaa vya matibabu wenye thamani zaidi ya shilingi milioni sita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

 

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni kutekeleza malengo, misingi ya upendo wa kiimani waliyorithishwa na Yesu Kristo kutoka kwa Mungu Baba, ambayo huitekeleza kila mwaka kwa ajili ya kusaidia wagonjwa (watoto) wenye uhitaji ili kuwapa faraja.

 

Akizunguzma katika makabidhiano hayo Hospitalini hapo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Kanisa la KKKT Usharika wa Boko, Mary Lema, amesema kusaidia watoto ni nadhiri yao kama wamama katika utumishi wao.

 

“Hii ni nadhiri tumejiwekea kila mwaka, sisi nadhiri yetu ni kwa ajili ya watoto, ni maombi yetu kwa Mungu, tuendelee kuwa sehemu ya hii huduma mpaka hapo mungu atakapoamua kutubadilishia muelekeo.

 

“Kipekee tunamsukuru Mungu kwa hii nafasi, tumeweza kuwa msaada katika kuchangia huduma kwa watoto wahitaji, tumekuwa tikifanya hii huduma, wamama wa ushirika wa boko  huu ni mwaka wa sita kwetu, tunaushukuru uongozi kwa kutupatia nafasi na kuwa nasi bega kwa bega.” Amesema na kuongeza kuwa.

 

“Wamama wamejitahidi, wametoa kiasi cha milioni 6,255,000 kuweza kukidhi matakwa ya mahitaji ambayo tulipewa kama orodha. Tumekuja sehemu ya wamama, sisi tuko wamama zaidi ya 900 kanisani.

 

“Asanteni sana, na tunashukuru uongozi wa Muhimbili, na tunashukuru pia uongozi wa kanisani kutupa kibali kushiriki na nyie kutupokea, asanteni sana na tunawapongeza kwa kazi nzuri ambayo mnaifanya bega kwa bega na Serikali, Mungu awabariki sana.

 

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi Hopsitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Redemptha Matindi, amewashukuru wamama hao na kuwataka watanzania wengine kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji ili kuwa sehemu ya kurejesha furaha kwa watanzania wenzao.

 

“Kwa namna ya pekee napenda kutoa shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbil, kitendo mlichokifanya au ambacho mmekuwa mkikifanya mara nyingi, cha kuguswa na kutoa msaada pale ambapo si kwamba mmezidiwa bali mnaguswa na kujali wengine, basi huo moyo uendelee na tutaendelea kuja kuwaomba.

 

“Kwa namna ya pekee ningependa kuiasaa jamii tujijengee utamaduni wa kuwasaidia wenzetu. Kikundi hiki cha hawa akina mama kimendelea kuwa msaada kwetu kwa muda mrefu sana na wamekuwa wakitusaidia kwa vitu vingi.” Amesema na kuongeza kuwa.

 

“Serikali pekeake haiwezi kukidhi kila kitu , wahitaji ni wengi kama si mtu mmoja mmoja kwenye jamii akiwiwa kidogo anachojaliwa akilete kusaidia wenzetu litakuwa jambo la busara na jambo jema. Na uwe ni utamaduni wa kila mtanzania.” Amesema ……..

 

Miongoni mwa vitu vilivyokabidhiwa ni

friji ya dawa yenye thamani ya laki saba, neutrition pump 2,500,000, mashuka yenye thamani ya 1,425,000. Mapazia yenye thamani ya Tsh 375,000, mafuta ya kupaka ya Viseline yenye thamani ya Tsh, 200, 000. Dawa za kutuliza maumivu ya panadol Tsh 275,000 pamoja na troli ya kubebea mashuka ambapo vitu vyote vinathamani ya Tsh 6,255,000.

 

Naye Mchungaji Msaidizi KKKT Usharika wa Boko, Mussa Nataniel Lucas kwa Niaba ya mchungaji Mkuu, amesema vitabu vya Mungu vinatufudisha upendo hivyo kutoa msaada ni moja ya misingi ya kuonyesha upendo kwa watu wengine wenye uhitaji.

No comments:

Post a Comment

Pages