Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Mohamed Omary Mchengerwa amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watalii wanaotembelea makumbusho na maeneo ya malikale nchini.
Mhe Mchengerwa ameyasema hayo leo bungeni Dodoma alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio na bajeti ya mwaka 2023/24 kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Amesema wageni wanaotembelea makumbusho na malikale wameongezeka kutoka 508,280 mwaka 2021/22 na kufikia wageni 887,285 kwa mwaka 2022/22.
Amewataka Watanzania kuendelea kujenga utamaduni wa kutembelea makumbusho na malikale.
Aidha, Mhe. Mchengerwa
amewapongeza wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania kwa jitihada wanazozifanya za maboresho na mageuzi yaliyopelekea ongezeko la wageni kwenye vituo vya Makumbusho na Malikale.
No comments:
Post a Comment