HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2023

SERIKALI TCU KUFUTA SHAHADA ZA KUEGELEZEA, PhD, UDHAMILI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga Warsha ya kubadilishana uzoefu kwa wenyeviti na wajumbe wa mabaraza, seneti na bodi za vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki iliyofanyika ukumbi wa APC Hotel and Conference Centre - Bunju, Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe, akizungumza katika Warsha ya kubadilishana uzoefu kwa wenyeviti na wajumbe wa mabaraza, seneti na bodi za vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki iliyofanyika Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Prof. Charles Kihampa, akizungumza wakati wa Warsha ya kubadilishana uzoefu kwa wenyeviti na wajumbe wa mabaraza, seneti na bodi za vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki iliyofanyika Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ambaye pia ni  waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Zakia Meghji akiwa katika Warsha hiyo.


 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (katikati) akifafanua jambo wakat akizungumza na waandishi wa habari katika Warsha ya kubadilishana uzoefu kwa wenyeviti na wajumbe wa mabaraza, seneti na bodi za vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki iliyofanyika ukumbi wa APC Hotel and Conference Centre - Bunju, Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe na kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Prof. Charles Kihampa. 


 

Na Mwandishi Wetu

 

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Mamlaka ya Vyuo Vikuu nchii TCU, wamekuja na mpango wa kufuta Shahada ya Udhamili na Udhamivu kwa wale walio egelezea kuzipata.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda katika Warsha ya kubadilishana uzoefu kwa wenyeviti na wajumbe wa mabaraza, seneti na bodi za vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki iliyofanyika ukumbi wa APC Hotel and Conference Centre - Bunju, Dar es Salaam.

Mkenda amesema TCU wamepata  utaratibu mzuri wa kugundua wale wanao egelezea kuandaa repoti zao huku akisisitiza kuongezeka umakini wa kusoma ripoti hizo.

"Niliwaagiza TCU tutumie mfumo wa kujua ni watu wangapi  walipoandika tafiti zao wali egelezea kwa watu wengine.

"Ni kuwa na utaratibu mzuri wa kugundua hilo lakini tunatakiwa tuongeze umakini wa kusoma na tukikuta Mtu amepata PhD ama Shahada ya Udhamili kwa kuegelezea tutafuta hiyo PhD ama Shahada ya Udhamili na kukitangaza chuo husika kuwa hakifanyi vizuri" amesema Waziri na kuongeza kuwa.

"Tumezungumza kuhakikisha kwamba wahitimu wetu wanakizi mahitaji ya watu katika ngazi zote kwa mfano jambo ambalo niliwaagiza TCU na wamelifanyia kazi.

"Kama unaenda kusomea Shahada ya Udhamili na PhD katika hivi Vyuo vyetu, kabla hujapata unatakiwa kutoa utetezi wa utafiti wako kwa njia mbili moja na wakuufunzi ama ya utetezi wa wazi ambayo ndio imepitishwa na TCU Ili mtahiniwa akiwa anajitetea awe anaulizwa maswali hadharani." Amesema Waziri Mkenda.

Waziri Mkenda amebainisha kuwa utaratibu huo sio kwa Tanzania pekee bali ni Dunia nzima hivyo ni sawa kutumika kama amabvyo Mataifa mengine yanautumia.

No comments:

Post a Comment

Pages