HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 27, 2023

CEO SINGIDA FOUNTAIN GATE FC AKOSHWA NA TIZI HUKO ARUSHA

Na John Marwa

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Singida Fountain Gate FC Olebile Sikwane amefurahishwa na maandalizi ya kuelekea msimu ujao wa mashindano ni mara baada ya kuwasili kambini jijini Arusha ambako kikosi chao kimeweka kambi.



Sikwane rai wa Botswana alitambulishwa wik kadhaa zilizopita na uongozi wa Klabu hiyo kuwa Mtendaji Mkuu ndani ya walima Alzeti hao wa Singida.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu na kupitia mitandao yao ya kijamii imeeleza kuwa.

 
"Mtendaji Mkuu, Olebile Sikwane, amefika kambini Arusha kujionea maandalizi ya msimu wa 2023\/24 yanayoendelea" pia imemnukuu kuwa.


"Nimefurahi kufika kambini. Nimefurahi zaidi kusikia Makocha wanasema wanaridhishwa na kiwango kinachooneshwa na wachezaji wetu. Tujiandae kwa msimu wenye neema" - CEO Sikwane.


No comments:

Post a Comment

Pages